Mohammed Dewji ametoa zaidi ya billion 1.3 bonus kwa ushindi kwa Simba

Mohammed Dewji ametoa zaidi ya billion 1.3 bonus kwa ushindi kwa Simba

carbohydates

JF-Expert Member
Joined
Oct 13, 2026
Posts
260
Reaction score
607
Raisi wa heshima wa klabu ya Simba Mohamed Dewji ameendelea kuihakikishia Simba maandalizi bora, ndani na nje ya Tanzania huku akiweka nguvu kubwa katika kuwapa mashabiki nafasi ya kufurahia na kusherehekea mapenzi hatua kubwa kwa timu yao.

Siju ya Jana Wanasimba walikutana pamoja Mwenge kutazama mechi yao ya CAF CL kwenye Big Screen , huku Wachesaji wakizawadiwa Milioni 200 za bonus baada ya ushindi , bado kuna Milioni 200 nyingine inawasubiri kama watashinda mchezo wa Wikiendi hii.

Hadi kufikia leo Dewji ametoa zaidi ya Bilioni 1.3 kama bonus kwa mechi chache ambazo Simba walihitaji hamasa zaidi

Chanzo : Shaffih Dauda
 
Aliye karibu na Mo amwambie kuwa bonasi anazotoa sawa lakini kama hatasajili wachezaji wa kiwango cha CAF CL hizo bonasi ni kazi bure tu kwani ataishia robo kama kawaida yao. Kwa mfano sasa hivi Simba haina mshambuliaji asili wa kati wa kiwango cha CAF ukimwacha Mpanzu peke yake. Ikitokea bahati mbaya Mpanzu kaumia, au akipata kadi au akikutana na mabeki wanaotumia nguvu mwanzo mwisho Simba itatetereka sana kwenye safu yao ushambuliaji.
 
Tajiri ana mahesabu yake nyie furahieni tu hizo pesa🤣🤣🤣🤣

Mahesabu ni kawaida. Hakuna mtu mwenye akili timamu anatoa pesa bila mahesabu. Sisi GSM huwa anatoa sana bonus tena wakati mwingine tunapiga hadi soup na chapati
 
Raisi wa heshima wa klabu ya Simba Mohamed Dewji ameendelea kuihakikishia Simba maandalizi bora, ndani na nje ya Tanzania huku akiweka nguvu kubwa katika kuwapa mashabiki nafasi ya kufurahia na kusherehekea mapenzi hatua kubwa kwa timu yao.

Siju ya Jana Wanasimba walikutana pamoja Mwenge kutazama mechi yao ya CAF CL kwenye Big Screen , huku Wachesaji wakizawadiwa Milioni 200 za bonus baada ya ushindi , bado kuna Milioni 200 nyingine inawasubiri kama watashinda mchezo wa Wikiendi hii.

Hadi kufikia leo Dewji ametoa zaidi ya Bilioni 1.3 kama bonus kwa mechi chache ambazo Simba walihitaji hamasa zaidi

Chanzo : Shaffih Dauda
Hizo zote kanaziweka kwenye hisa za Simba, mwisho wa siku katasema kanawadai simba
 
Back
Top Bottom