Replica
JF-Expert Member
- Aug 28, 2017
- 1,681
- 8,887
Mfanyabiashara, Mohammed Dewji wiki hii alianza kampeni yake ya 'Mo Cares' akiielezea kama Moo anajali watanzania ikiwemo kuwapa zawadi washindi wataojibu maswali yake. Dewji anasema alitekwa miaka mitano iliyopita na wasiojulikana na anawashuru watanzania wote waliomuombea.
Miongoni mwa maswali aliyouliza ni muanzilishi wa kampuni ya Moo lakini alianza na kutoa elimu juu ya kurithi. Moo amesema urithi ukitoka kwa baba kwenda kwa mtoto ni asilimia 50 tu ndio huwa wanafanikiwa kwenye maisha yao na ni asilimia 5 pekee ya wajukuu wanafanikiwa akimaanisha mali za urithi hupotea na wahusika kuanza upya.
Dewji amesema kurithi ni vizuri lakini pamoja na kurithi zinakuja responsibilities ya kuzikuza. Amesema yeye anashukuru alilirithi lakini ameweza kuzizidisha fedha hizo maradufu ikiwemo kufanya kazi kwa jitahada na nidhamu ya hali ya juu.
Amewaasa wanaorithi inabidi wajitume ili wafanikishe.
Mwisho Moo alitoa jibu mwenyewe kwa kumtaja muanzilishi wa Mohammed Enterprise kuwa ni bibi yake anayeitwa Fatma Hassanali Fazal Dewji na alianzisha biashara hiyo mikoa ya Singida, Dodoma na Arusha na baadae baba yake Ghulam Dewji alipokea kijiti na baadae kumpa yeye Moo mwaka 1998.