SAYVILLE
JF-Expert Member
- Mar 25, 2010
- 7,895
- 12,975
- Thread starter
- #41
Watu wana mihemko, wanadhani nimeanza kumuangalia MH mechi ya juzi. Hayo yote unayosema ni sahihi kabisa.Kuna wachezaji Simba Wana bahati ya kupendwa mkude na Mohamed husein ila wote hao Wana mapungufu makubwa.
Sifa kubwa ya Shabalala ni kupendwa kushambulia lakini mipira yake mingi ya mwisho haiendi inapotakiwa sababu anapenda kukaa na mpira muda mrefu na anapoamua kupiga tayari adui anakuwa amejipanga.
Pasi zake nyingi za uchonganishi, anaweza kuacha kutoa pasi Kwa mchezaji ambaye hajakabwa lakini akatoa pasi Kwa mchezaji aliyekabwa na watu 3.
Hana kasi na anapata shida sana anapokutana na winga mwenye kasi pia ana tabia ya kukaba Kwa macho.
Kuna wakati mchezaji ambao walikuwa tegemeo kwa timu lakini kutokana na umri au sababu zingine, kiwango kushuka na anakuwa mzigo zaidi kwa timu. Kwa wachezaji wa namna hiyo ambayo na wewe umesema, inakuwaga ngumu kuwaacha mara moja, kama ilivyotokea kwa Kagere, kwa hiyo si vibaya kuwaazishia benchi na wakawa wanaingia pale madhaifu yao yanapokuwa siyo risky sana.
Tatizo hawa seniors hata nje ya uwanja ni shida huko makambini na wakati mwingine ndiyo vyanzo vya migogoro, ungesema wangeweza kuwa msaada kuwajenga wachezaji wapya kwenye timu.