The Watchman
JF-Expert Member
- Nov 7, 2023
- 2,186
- 4,940
Mwenyekiti wa UVCCM Taifa, Mohammed Ali Kawaida ametoa maagizo kwa Viongozi wa UVCCM Mikoa yote na Wilaya zote Tanzania kuwa na vitega uchumi ili kuondoa utegemezi.
Kawaida ameyasema hayo jana March 24, 2025 Mkoani Singida alipofanya ziara ya kufungua vitega uchumi vya UVCCM ikiwemo fremu 73 za maduka ya biashara na jengo la hosteli za kisasa lenye vyumba 19 ambavyo vitatumiwa na Wanafunzi wa Chuo cha St. Joseph tawi la Singida, ambapo ameongoza uzinduzi huo akiwa na Mwenyeji wake Mwenyekiti wa UVCCM Mkoa wa Singida, Zulfat Ally Muja.
Kawaida amesema “Nitoe wito kwa wale ambao mmeanza kutekeleza sera hii basi waendelee, kwa wale ambao hamjaanza watekeleze sera hii ya Umoja wa Vijana na Uchumi Imara, utekelezaji wa sera hii unawezekana kwakuwa Serikali imeweka mazingira mazuri kwa Vijana kuweza kuanzisha shughuli zenye kuzalisha vyanzo vya mapato”
Kabla ya kufungua miradi hiyo, Kawaida alipokelewa katika eneo la Ikungi na kuongea na maelfu ya Wananchi ambao aliwaeleza kuelekea uchaguzi mkuu waendelee kuiamini CCM na Mgombea Mteule Dkt. Samia Suluhu Hassan ambapo pia amekabidhi gari lililotolewa na Mkuu wa Mkoa wa Singida, Halima Dendego na pikipiki sita zilizotolewa na Mbunge wa Singida Magharibi Elibariki Kingu kwa ajili ya Makatibu wa UVCCM Mkoa wa Singida ili wakatimize majukumu yao.