Mohammed Kawaida: Mliona tulichokifanya, mwingine ajifanye mkubwa kuliko CCM aone

Nilidhani Nchimbi Alijiuzulu. Sasa wanaanza kuthibitisha tetesi za utata wa barua yake ya kujiuzulu.
Wengine walikaa kimya ili tu wawe hai kama sasa..
Ule mwandiko haukua wake.
 
Sawa tu si ni chama chenu hampingwi muachieni Lissu sasa yeye ni wa chama kingine
Jamani si tulikubaliana kesi iendelee tu kwa kuwa Lissu ni Mwanasheria nguli na anawagaragaza tu mawakili wa serikali?
 
Hivi haka kakijana hakajui zama huwa zinabadilika? Kamechemka kama moto wa kifuu, kanajua mama yao atadumu milele kukabeba zaidi, kakumbushwe mbeleko huwa inachakaa na inakosa uwezo wa kubeba hata kichanga

Mganga huwa anakufa pia sio immortal
 
Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Taifa Mohamed Kawaida ametoa onyo kali kwa viongozi wa serikali na wa Chama hicho wanaojifanya kuwa ni wakubwa kuliko chama hicho kwamba hawatasita kuwachukulia hatua

Soma pia >> Kawaida: Kamati Kuu ilimuita Nchimbi lakini kwa sababu ya kiburi na kudharau chama aligoma kuja, tukamfukuza

Amesema “Anayetaka kujifanya yeye ni mkubwa kuliko CCM, tulichokifanya juzi ni mfano"

Mwenyekiti huyo wa UVCCM Taifa, Mohammed Ali Kawaida, ametoa kauli hiyo leo, Septemba 12, 2026, akiwa katika ziara yake mkoani Mbeya.

Amesema hakuna mtu aliye mkubwa kuliko Chama, akisisitiza kuwa matukio ya hivi karibuni ni mfano wa nguvu na uwezo wa CCM katika kusimamia mambo yake.

1. Polepole
2. Nchimbi
3. Mohammed Kawaida
 
Kuna msemo kwamba ukicheka na nyani utavuna mabua. Nchimbi akiwa Katibu Mkuu alikuwa na nafasi ya kufanya usafi kwenye hicho chama badala yake akaendelea kuleta ukondoo hadi na yeye wamemgeuza kuwa kondoo wa kafara.
 
Back
Top Bottom