TANZIA Mohammed “Muddy Physics” wa Mchikichini afariki dunia

Inna lillahi wa illahi rajiuun. Mtu aliyefundisha Physics na kuifanya kuonekana rahisi.
 
Pia niliwahi kufundisha mchikichi japo sikufanikiwa kupata jina kwani nilifundisha muda mfupi sana.
 
Duuu! Aisee apumzike kwa amani. Kila nikitazama jinsi nilivyopitapita kwenye safari yangu ya kielimu siwezi kusahau mahali panapoitwa mchikichini na pia siwezi kumsahau huyu jamaa alinisaidia sana kwenye physics.
Kwa kweli hata mimi siwezi kusahau Mchikichini. RIP Muddy.
 
Kwa taarifa niliyoisikia muda si mrefu ni kuwa:

Yule aliyekuwa mtabe aliyekabidhiwa utabe wa physics pale Mchikichini, MUDY PHYSICS AU COMMISSIONER....
Mtaalam wa physics ndo alikuwa anamiliki gari ya hivi huku kina mondi wasokuwa hata na cheti wanamiliki magari ya kifahari. Endeleeni kuwekeza kwenye utumwa wa elimu.
 
Safi mkuu huo ndio ubinadamu
 
2005 o level and 2008 A level( I think topic 1)
His last words were always “ladies and gentlemen, let’s end here for this particular juncture of today, soooo astalavista manyanaaaa”
Ndio maisha.
 
Kwa hisani yako naomba maelekezo ya mlipomlaza mwalimu wangu nataka nikirudi Tanzania niende kwwenye kaburi lake, niubusu mchanga wake na nimuombee dua, kipenzi cha wanaadamu, mwanachuoni wa zama zetu katika ilmu ya fisikia.
 
RIP muddy Mambo yalkua yakinikamata kwenye Muncaster na nelkon nakimbilia kwenye vitini vyako...
Umeniongelea na mimi na wala siongezi neno. Mwenyezi Mungu muangalie kwa jicho la huruma kiumbe wako huyu. Amekuja kwako mnyonge na dhalili, basi msamehe alipoteleza, kwa rehma zako ya Allah
 
Mtaalam wa physics ndo alikuwa anamiliki gari ya hivi huku kina mondi wasokuwa hata na cheti wanamiliki magari ya kifahari. Endeleeni kuwekeza kwenye utumwa wa elimu.
Kwa hiyo wote tuwe kama akina Mondi? Unaita elimu utumwa cha ajabu watoto wako umewapeleka shule baada ya kuwaacha nyumbani,ukiumwa unaenda hospitalini sasa sijajua huko hospitalini unatibiwa na Mondi.
 
Vp Kuna kiongozi yoyote amezungumzia ama kutoa pole kwenye huu msiba wa muddy fizikia!

Naona kimyaaaaa?

Ila angekuwa msanii au Hawa wazushi wa kuuza sura
Mjini mngeona pole za kumwaga

Ova
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…