Sasa nafunga mjadala. Nakubaliana na wewe kuwa mapinduzi yalifanywa na Tanganyika na kuwa kulikuwa hakuna sababu yakufanya mapinduzi, kwani hakuna aliyekuwa akidhulumiwa chini ya utawala wa Sultani na kuwa SMZ na sio utawala wa Sultani ndio yenye dhulma kila corner, kuanzia kwenye elimu na kwengineko. Pia, nakubaliana na wewe kuwa nia ya kuipindua serikali ya Sultani ilikuwa kuuangamiza uislamu Zanzibar FULL STOP!
Mjadala umeisha. Sitojibu tena!
Ngida 1,
Si lazima ulete majibu ukisoma peke yake pia inatosha huenda kama wewe
ni Muislam unatanabahi na ukawaidhika.
Kuna wakati kwa hakika mtu unashangazwa unapoona juhudi hadi za kuua
wananchi alimuradi Zanzibar ibakizwe kwenye mikono ya kundi fulani wenyewe
wanajiitikadi ni ''Wanamapinduzi Daima.''
Zanzibar ni nchi ya Kiislam.
Tanzania Bara Waislam ni wengi lakini ukweli ni kuwa hawako katika sehmu nyingi
sana za maamuzi hivyo ni shida sana kwao kuwa na athari katika utawala.
Waislam kwa uchache wao katika Bunge walishindwa kuzuia Sheria ya Ugaidi kupita.
Unaweza kupata mengi hapo chini:
Mohamed Said: YALIYOTOKEA TANZANIA BAADA YA KUPITISHWA SHERIA YA UGAIDI 2
Manipulation of State Laws and Government Policies
Crusade Against ‘Radical Islam’ in Tanzania
Excerpts from ‘’Islam, Terrorism and African Development’’
University of Ibadan, 2006
by Mohamed Said
Hata umoja wao BAKWATA wameundiwa na hadi leo baada ya miaka 50 bado ni
mjadala hajulikani nani kaunda BAKWATA.
Zanzibar haijaweza kujiepusha na ukweli huu.
Angalia historia ya visiwa katika chaguzi zote zilizopita utapata jibu.
Kipi kilichoudhi Bara wakati Zanzibar ilipojiunga na Organisation of Islamic Conference
(OIC) mwaka 1993 kiasi cha kulazimishwa lazima Zanzibar ijitoe OIC?
Tafadhali ingia hapa usome sakata la Zanzibar na OIC:
Mohamed Said: Zanzibar Membership to Organisation of Islamic Conference (OIC) and
Islam in Africa Organisation (IAO)
Ukiweza kutafakari katika haya utaweza kujua kwa nini kulikuwa na vurugu Bunge Maalum
la Katiba na kwa nini Bunge la Tanzania linahodhiwa na watu fulani?
Iweje pawepo katika jamii wale wenye kuweza kujiimarisha zaidi kwa kujiongezea wafuasi
zaidi katika bunge hilo?
Kwa kuwa wewe umeleta suala la Uislam sasa zingatia hayo hapo chini:
Bunge la Katiba lilikuwa na uwiano katika nyanja zote isipokuwa ya dini.
Chunguza nani lazima kama ada wawe wachache na nani wawe wengi.
Haya yote ni kutaka na kutafuta nini?
Wazanzibari kama Waislam watakuwa na salama gani huko mbele tuendako?
Hebu ingia hapa uone upogo huu:
Mohamed Said: Uteuzi wa Baraza la Katiba Haukuzingatia Uwiano wa Kidini Waislam Kama
Ada Wamepunjwa
Sasa kwa kuhitimisha ili picha ikae sawa ukutani ingia hapa chini ujikumbushe wapi
Zanzibar imetoka katika kutafuta uhuru wake katika historia ya miaka ya hivi karibuni:
Mohamed Said: Hofu ya Uislam Kuwa na Nguvu Zanzibar ya Serikali Tatu
Ngida 1,
Kuna ndugu yangu kakujibu kasema nimekupuuza ndiyo maana sikukujibu.
Ukweli ni kuwa nimekukwepa lakini nimeona nikurejee baada ya wewe kusema mimi
sina majibu ya kukujibu wewe.
Jibu utakuwanalo wewe na wasomaji kama mimi nina majibu au sina.
Ikiwa hujasoma kitabu hiki kisome kitakupa majibu ya yale uliyofananisha ya watu kupoteza
maisha yao kwa kudhulumiwa roho zao na hilo usemalo, ''kunyimwa elimu.''