Mohammed Said na Mapinduzi ya Zanzibar

Hapana tatizo, Endelea Kuenjoy uhuru wa CCM. mzee Mohamed Said alikufahamu mapema ndio mana akakupuuza.

Hajanipuuza lakini niliyoyaandika asingeweza kuyapinga.
Utapingai vipi kusema kama waafrika walidhulumiwa kielimu chini ya usultani?
 

Naona Chief hujafahamu hapa tunazungumza nini. Tushakubaliana huko nyuma kuwa mapinduzi ya Zanzibar yalipata msaada kutoka nje.

Tunachobishana hapa na wana-historia na ambacho kililetwa mwanzo as term of reference ni kama chini ya usultani dhulma zilikuwepo zidi ya waafrika au laa? Mfano ukatolewa wa kwenye elimu - hichi ndicho tunachokizungumza na sio nanai alitusaidia kupindua. Hope the issue is clear to you now!

Halafu unamzungumza Karume, suala langu ni kuwa ukimjua Karume? Uliwahi kukutana nae uso kwa uso? Ulikuwa angalau miaka 18 pale alipouliwa ile 1972? Karume huwezi kumjua kwa kusoma vitabu au kuhadithiwa na wana-historians.

Angelikuwa hai waziri wa fedha wa Mwalimu (Ndugu Amir Jamal) ningelikuomba umuulize eti Karume ni nani au ungelimuuliza yalimkuta nini pale alipotaka kuziweka pesa za kigeni za Visiwani na Bara chini ya Central Bank moja ya BoT?

Au kama Mwalimu nae angelikuwa hai ningelikuomba umuulize alijibiwa nini na Karume alipomuuliza Sheikh Karume mbona mnaowaowa tu huko Visiwani? Au alisema nini Karume pale Mwalimu alipotangaza Azimio la Arusha kule Bara?

Karume alikuwa ni mtu mwengine na hata hawa historians wetu wanalijua hilo na kulikubali. Angelikuwepo mpaka leo, either tungelikuwa ni nchi moja au angeshauvunja Muungano wenyewe au tungelibakia na mambo ya Muungano yale yale ya 1964.

Anyway, ngojea nikusaidie kidogo. Unamjua dada FATMA KARUME ambae ni Rais wa Tanganyika Law Society? Basi kama unamjua da Fatma, toa sura yake ya kike na weka sura ya kiume na utakuwa ushampata Karume!
Huyu dada ndie aliemrithi Karume kwa hali zote. Kwa sisi tunaemjua Karume, huyu dada ni Karume mtupu and she is going to be the next big thing in Tanzania!
 
Ngida1

Tunachotaka ni uthibitisho wa hiyo dhulma mnayoizungumza. Sio mutulazimishe kuamini kwa maneno.

Nakuhusu kusaidiwa na Tanganyika mapinduzi. Mkuu ASP hawakusaidiwa mapinduzi na Tanganyika bali Tanganyika ndio waliofanya mapinduzi hivo nivitu viwali tafauti jaribu katafautisha na ndio mana nilikuuliza swali mwenye mapinduzi ni nani ambalo ulishindwa kuniaambia. Wengine wanasema Okello, wengine wanasema comrade, wengine wanasema umoja wa vijana ASP, Alimradi wanakorogana tu. Kama tanganyika alisaidia huyo aliesaidiwa ni nani?

Sijamuona Karume, Lakini nimejiridhisha vya kutosha kutokana na ufahamu wangu kwake. Nimeshafanya mahojiano ya ana kwa ana kwa zaidi ya watu 6 wanaomfahamu vizuri karume. mbali niliyosoma mengi kutoka kwa wengine. Bado munstragle mpaka leo kuthibitisha ushiriki wake katika mapinduzi, munabakia kumwita jemedari!!!!!!! labda wa udongo.
 

Sasa nafunga mjadala. Nakubaliana na wewe kuwa mapinduzi yalifanywa na Tanganyika na kuwa kulikuwa hakuna sababu yakufanya mapinduzi, kwani hakuna aliyekuwa akidhulumiwa chini ya utawala wa Sultani na kuwa SMZ na sio utawala wa Sultani ndio yenye dhulma kila corner, kuanzia kwenye elimu na kwengineko. Pia, nakubaliana na wewe kuwa nia ya kuipindua serikali ya Sultani ilikuwa kuuangamiza uislamu Zanzibar FULL STOP!
Mjadala umeisha. Sitojibu tena!
 

usikasirike mkuu, ulikuja kwa mjadala nao unapandisha
 
Dos,
Nimeingia Maktaba nimekuta hii orodha ingawa majina mengine
uneshayataja:
  1. Aboud Jumbe
  2. Dr Kingwaba
  3. Ali Khamis
  4. Othman Sharif
  5. Kassim Hanga
  6. Mohamed Ghassany
  7. Ali Muhsin Barwani
  8. Tahir Adnan
  9. Nassor Abdallah
  10. Sanura Shaqsi
  11. Asya Amour
  12. Said Shaqsi
  13. Ibrahim Noor
Naendelea In Shaa Allah kutafuta majina mengine...
  1. Abdulaziz Twala
  2. Abdulwakil Nombe
  3. Haji Abdulaziz
 
Ngida 1,
Si lazima ulete majibu ukisoma peke yake pia inatosha huenda kama wewe
ni Muislam unatanabahi na ukawaidhika.

Kuna wakati kwa hakika mtu unashangazwa unapoona juhudi hadi za kuua
wananchi alimuradi Zanzibar ibakizwe kwenye mikono ya kundi fulani wenyewe
wanajiitikadi ni ''Wanamapinduzi Daima.''

Zanzibar ni nchi ya Kiislam.

Tanzania Bara Waislam ni wengi lakini ukweli ni kuwa hawako katika sehmu nyingi
sana za maamuzi hivyo ni shida sana kwao kuwa na athari katika utawala.

Waislam kwa uchache wao katika Bunge walishindwa kuzuia Sheria ya Ugaidi kupita.
Unaweza kupata mengi hapo chini:
Mohamed Said: YALIYOTOKEA TANZANIA BAADA YA KUPITISHWA SHERIA YA UGAIDI 2
Manipulation of State Laws and Government Policies
Crusade Against ‘Radical Islam’ in Tanzania
Excerpts from ‘’Islam, Terrorism and African Development’’
University of Ibadan, 2006
by Mohamed Said

Hata umoja wao BAKWATA wameundiwa na hadi leo baada ya miaka 50 bado ni
mjadala hajulikani nani kaunda BAKWATA.

Zanzibar haijaweza kujiepusha na ukweli huu.
Angalia historia ya visiwa katika chaguzi zote zilizopita utapata jibu.

Kipi kilichoudhi Bara wakati Zanzibar ilipojiunga na Organisation of Islamic Conference
(OIC) mwaka 1993 kiasi cha kulazimishwa lazima Zanzibar ijitoe OIC?

Tafadhali ingia hapa usome sakata la Zanzibar na OIC:
Mohamed Said: Zanzibar Membership to Organisation of Islamic Conference (OIC) and
Islam in Africa Organisation (IAO)


Ukiweza kutafakari katika haya utaweza kujua kwa nini kulikuwa na vurugu Bunge Maalum
la Katiba na kwa nini Bunge la Tanzania linahodhiwa na watu fulani?

Iweje pawepo katika jamii wale wenye kuweza kujiimarisha zaidi kwa kujiongezea wafuasi
zaidi katika bunge hilo?

Kwa kuwa wewe umeleta suala la Uislam sasa zingatia hayo hapo chini:

Bunge la Katiba lilikuwa na uwiano katika nyanja zote isipokuwa ya dini.
Chunguza nani lazima kama ada wawe wachache na nani wawe wengi.

Haya yote ni kutaka na kutafuta nini?
Wazanzibari kama Waislam watakuwa na salama gani huko mbele tuendako?

Hebu ingia hapa uone upogo huu:
Mohamed Said: Uteuzi wa Baraza la Katiba Haukuzingatia Uwiano wa Kidini Waislam Kama
Ada Wamepunjwa


Sasa kwa kuhitimisha ili picha ikae sawa ukutani ingia hapa chini ujikumbushe wapi
Zanzibar imetoka katika kutafuta uhuru wake katika historia ya miaka ya hivi karibuni:

Mohamed Said: Hofu ya Uislam Kuwa na Nguvu Zanzibar ya Serikali Tatu

Ngida 1,
Kuna ndugu yangu kakujibu kasema nimekupuuza ndiyo maana sikukujibu.

Ukweli ni kuwa nimekukwepa lakini nimeona nikurejee baada ya wewe kusema mimi
sina majibu ya kukujibu wewe.

Jibu utakuwanalo wewe na wasomaji kama mimi nina majibu au sina.

Ikiwa hujasoma kitabu hiki kisome kitakupa majibu ya yale uliyofananisha ya watu kupoteza
maisha yao kwa kudhulumiwa roho zao na hilo usemalo, ''kunyimwa elimu.''

 
USIOPINGIKA kwa utawala uliyopita wa Sultani na kwa tawala zetu za sasa pia.
Hapa umeonesha kidogo kufahamu sehemu ya ukweli,lakini bado kidogo kuhusu elimu.

Ujuwe kuwa Agustino Ramadhani Alisoma Zanzibar?na ndo alikuwa Muanzilishi wa AA(African Association) sasa sijuwi waafrika gani hao unao wasema kuwa hawa kupewa elimu?

Mbona hata huko Tanganyika kulikokuwa na Watawala Malaika (wazungu) pia nao walitowa elimu kimtindo mtindo ,wengi waliosoma walikuwa wahindi,na jamii za watu wa Mijini? Hili je hulisemi?

UJUWE KUWA MUINGEREZA NDO ALIUWA MTAWALA NA NDO ALIETOWA ELIMU.
NA BAADHI YA JAMII ZILIJIJENGEA mASHULE YAO.

Hata hao waarabu wengi walikuwa hawkusoma kabisa .
 
KUDUME CHENYEWE KUMBE CHA GARI YA NGOMBE!, Maana naona pesa imechukuliwanchi imechukuliwa,na Azimio la Arusha limekujaZNZ na Hata mwenge wa Uhuru wa Tanganyika unakimbizwa Zanzibar kila mwaka,kama vile tulivyo kuwa tukisheherekea Siku ya Malkia wa UK hapa ZNZ enzi zile unazosema za Mkoloni Sultani.
Sasa sijui Kidume Alikuwa Nyerere au Mzee K?
 
Leo tarehe 12 January ni Sikukuu ya Mapinduzi ya Zanzibar, nachukua nafasi hii kuwatakia nyote heri na fanaka za Mapinduzi na kukutakieni maadhimisho mema ya sherehe ya kumbukumbu ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar kwa watakao shereheka kwa wale wenye kumbukumbu njema, na kwa vile Mapinduzi Matukufu yale pia yaliandamana na umwagaji damu, natoa pole kwa wenye kumbukumbu chungu.
P
 
Nawasalimu katika jina la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, na kuwatumia salaam zangu za kuadhimisha kumbukumbu ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar.

Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar, tutayalinda kwa gharama yoyote.

Nawatakia maadhimisho mema ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar.

Kazi Iendelee!.

Paskali
 
Mkuu una mahaba mno na mapinuzi yenu
 
Mkuu una mahaba mno na mapinuzi yenu
Huu ni uchokozi, Mapinduzi Matukufu ni ya Zanzibar, ila kwavile sasa tumeungana, tumekuwa kitu kimoja, hivyo Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar pia ni yetu na ndio maana tumeapa tutayalinda kwa gharama yoyote.
P
 
Huu ni uchokozi, Mapinduzi Matukufu ni ya Zanzibar, ila kwavile sasa tumeungana, tumekuwa kitu kimoja, hivyo Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar pia ni yetu na ndio maana tumeapa tutayalinda kwa gharama yoyote.
P

Sasa kwanini huko Zanzibar wanapata tabu sana kuyaenzi? viwanjani huwa wanajaza vikosi vya ulinzi pamoja na kulzimisha wanafunzi na walimu wa maskuli ya serekali ili wazibe mapengo, Wanalazimisha wafanya biashra waeka mabendera kwenye maeneo ya biashara zao. Mbona wananchi wameyakataa hayo mapinduzi mkuu?
 
Endelea kusema wameyakataa ! leo ni miaka 58, itafika hadi miaka 100!.
P
 
Mapinduzi yalilenga kulinda maslahi ya Mwingereza,kanisa Katoliki,Anglikana na maslahi ya akina Rothchild.Nyerere aliagizwa ahakikishe anapindua na kisha sultan Jamshid ampokee halafu atapewa hifadhi Uingereza ili asifurukute.Hii ni sawa na alivyofanyiwa Jumbe,Kabudi na William Vangimembe Lukuvi.Chifu Hangaya ,Mungu anakuona.
 
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…