Labani og
JF-Expert Member
- Sep 15, 2020
- 19,637
- 29,473
Ni takribani kilometa 5,627 kutoka katikati ya mjini mkuu wa misri Cairo mpaka katika jiji kubwa la London pale nchini Uingereza hakika ni umbali mrefu lakini nani anajali kama unaenda kupambana kutafuta maisha.
Alitokea katika ardhi yenye historia kubwa zaidi duniani ardhi yenye historia pia ya utawala ardhi yenye kila aina ya mambo ya kihistoria hapa simzungumzii mwingine Bali namzungumzia fundi wa mpira na nyota wa sasa wa club ya Liverpool mohamed sallah nyota anayetikisa dunia kwa sasa.
Safari yake kisoka alianzia katika club ndogo sana nchini misri club iliyofahamika kwa jina la All mokawloon , kipindi salla anatoka na kwenda katika club hiyo nani alijua kuwa ipo siku atakuwa mfalme mpya ndani ya taifa la misri maana wamepita wachezaji wengi wakubwa sana na waliotikisa kama hassan shehata,mido, na wengine wengi kama kina aboutrika ni nani ambaye alijua kuwa salah ipo siku atakuja kutikisa na kuzima majina yote makubwa yaliyowahi kutokea misri.
Alianza kwa kucheza timu za misri za u20 ,u23 na katika mashindano flani ya timu za vijana mascot wa Basel ya uswiss walimuona na kumbeba na hata siku anaondoka nchini misri kwenda uswiss alinukuliwa akisema siku moja natamani nije kuwa mchezaji nayeibwa na kupendwa zaidi nchini misri.
Kuanzia hapo kilichokuja kutokea kinabaki bado historia kwani katika mechi mbili tu za club bingwa dhidi ya chelsea zilitosha kuonesha yeye ni nani na kilichokuja kutokea ni kocha wa wakati huo wa chelsea kumtaka na hatimaye alisajiliwa kwa pound 11.
Na hapo ndipo safari yake ya mo salah ilipoanza safari ya kutengeneza jina lake na ufalme wake japo safari yake ilikuwa ni safari iliyogubikwa na machungu na karaha ndani yake na kama angekuwa na moyo mlaini angeishia kurudi nyumbani kama kaka yake Amri Zhaki maisha yalivyomshinda pale Epl na kuamua kurudi nyumbani.
Maisha ndani ya Stamford Bridge hayakuwa mazuri kwani alijikuta akicheza mechi chache huku akifunga goli 3 tu katika mechi 13 alizocheza kiasi cha kupelekea kutolewa kwa mkopo katika timu kadhaa za Roma na Fiorentina nyote vikiwa ni vilabu vya italy na baada ya mkopo kuisha huku akiwa anafanya vizuri club ya Roma walilipa kiasi cha pound 15 na kumnunua mazima.
Siku zote waswahili huwa wanasema Muda ndo hakimu wa mambo yote baada ya kuonesha kiwango bora sana ilitosha kumfanya vilabu kadhaa vimtolee udenda na baada ya uvumi wa Muda mrefu hatimaye club ya Liverpool walimsajili kwa kiasi cha pound 42 kiasi ambacho kilipanda mpaka pound 50 kutokana na mafanikio na makombe ambayo angebeba clubuni hapo.
Kilichofuata baada ya usajili huo kinabaki kuwa historia muhimi kwake na kwa club yake makombe pamoja na kuvunja rekeodi za kila aina pamoja na tunzo binafsi kinamfanya salah kuwa mchezaji kipenzi maarufu zaidi nchini wingereza na hata duniani kwa ujumla huku timu ya taifa akiwasha moto huku clubuni akiwasha moto na kumfanya kuwa mchezaji bora kabisa kwa sasa epl na katika timu ya taifa na katika bara la africa kiujumla.
Japo mimi sio shabiki wa Liverpool huyu mwamba now anatisha