Taasisi ya Mifupa-MOI
Senior Member
- Apr 15, 2025
- 118
- 214
Taasisi ya Tiba ya Mifupa na Ubongo Muhimbili (MOI) imeeleza mpango wake wa kuanzisha huduma mpya mbalimbali za kibobezi zitakazoifanya kuendelea kuwa kitovu cha weledi cha matibabu ya mifupa na mfumo wa fahamu katika ukanda wa Afrika.
Akizungumza wakati wa uzinduzi wa maadhimisho ya miaka 30 ya MOI, Mkurugenzi Mtendaji wa MOI Mhe, Balozi Dkt. Mpoki Ulisubisya ameelaza, "Tumejipanga kuanzisha huduma ya Benki ya Mifupa, huduma za kibobezi za Upasuaji wa nyonga, magoti kwa kutumia Roboti, ubadilishaji wa viungo vya bega na kiwiko na upasuaji wa mifupa unyayo na kiwiko cha mguu.
Aidha, kwa upande wa huduma za mfumo wa fahamu, Dr. Mpoki amezitaja huduma hizo kuwa ni pamoja na upasuaji wa uti wa mgongo kwa kutumia Roboti, huduma kwa wagonjwa changamoto ya kutembea, maumivu sugu, Tiba ya mgongo kwa kutumia mbinu za kisasa.
Amesema MOI itaendelea kujikita katika kusogeza huduma zake katika mikoa ya Arusha, Mara, Kagera, Kigoma, Katavi,Njombe na Ruvuma Ili kuendelea kupunguza mlundikano wa wagonjwa MOI
Mhe Balozi ,Dkt. Mpoki amesisitiza kuwa Huduma za tiba Mkoba (Mobile Outreach Services) zitaendelea kutolewa katika mikoa mbalimbali nchini ili kuwafikia wananchi wengi zaidi.
“Tunataka kuhakikisha Watanzania wanapata huduma ambazo hapo awali zilikuwa zinapatikana katika vituo vichache duniani. Uwekezaji huu utaongeza ubora wa huduma na kutoa matumaini kwa wagonjwa wengi zaidi," alisema Dkt. Mpoki.
Dkt.Mpoki ameongeza kuwa huduma hizi mpya ni sehemu ya utekelezaji wa mpango mkakati wa taasisi ya MOI wa kuendelea kuwa kinara wa huduma za kibingwa na ubingwa bobezi barani Afrika.