Miss Zomboko
JF-Expert Member
- May 18, 2014
- 4,599
- 9,532
Taasisi ya Tiba ya Mifupa, Upasuaji wa Ubongo na Mishipa ya Fahamu Muhimbili (MOI), imesema imekuwa ikiwapoteza wagonjwa kati ya wawili hadi watatu kila mwezi katika Idara ya Wagonjwa wa Dharura kutokana na ajali zikiwamo za pikipiki.
Ofisa wa Takwimu wa MOI, Joshua Ngahyoma, aliiambia Nipashe jana jijini Dar es Salaam kuwa kuna kasi kubwa ya ongezeko la wagonjwa wa ajali wanaowapokewa na kulazwa kwenye taasisi hiyo, huku mwaka 2019 ukiwa na rekodi kubwa zaidi.
Alisema idadi ya wagonjwa hao wanaolazwa, wanaoongezeka kwa wastani zaidi ya mara tatu ya wale wanaotibiwa ma kuruhusiwa kulinganisha na takwimu za miaka mitatu mfululizo hadi mwaka juzi.
Ngahyoma alisema kuwa mwaka jana ilifikia mara nne ya idadi ya wagonjwa wanaotibiwa na kuruhusiwa, akibainisha kuwa kila mwaka MOI imekuwa ikipoteza wagonjwa wa dharura kati ya 28 na 35 wanaofikishwa hospitalini hapo.
“Wastani kwa mwaka wa vifo vinavyotokana na ajali ni kati ya 28 na 35, hivyo ni wastani wa vifo viwili hadi vitatu kwa mwezi. Hivi ni vifo vilivyotokea Idara ya Dharura,” alisema.
Alisema kuanzia mwaka 2016 hadi mwaka jana, walipokea wagonjwa wa ajali 34,863. Kati yao, waliotibiwa na kuruhusiwa ni 8,715 na waliolazwa ni 26,147.
Kwa mujibu wa takwimu hizo, kuna ongezeko la asilimia 38 au theluthi moja ya wagonjwa wa ajali wanaolazwa MOI, akifafanua kuwa ni kutoka wagonjwa 5,915 mwaka 2016 hadi kufikia wagonjwa 8,208 mwaka jana.
Alifafanua kuwa idadi ya wagonjwa waliopokewa mwaka jana, ilivunja rekodi ya kuwa zaidi ya mara nne ya waliopokewa miaka mitatu iliyotangulia, yaani kuanzia 2016 hadi 2018.
Ngahyoma alibainisha kuwa mwaka 2016, walitibiwa na kuruhusiwa wagonjwa 1971, waliolazwa walikuwa 5,915 na kufanya jumla ya wagonjwa waliopokewa mwaka huo kutokana na ajali kuwa 7,887.
Alisema kwa kipindi cha mwaka 2017, walitibiwa na kuruhusiwa wagonjwa 1,937, waliolazwa 5,811 na kufanya ya waliopokewa MOI mwaka huo kuwa 7,748.
“Mwaka 2018, waliotibiwa na kuruhusiwa walikuwa 2,071 na waliolazwa 6,213 na jumla kuwa wagonjwa 8,284 waliopokewa mwaka huo,” alifafanua.
Aliongeza kuwa kwa mwaka jana, waliotibiwa na kuruhusiwa wagonjwa 2,736, waliolazwa 8,208 na kufanya jumla ya waliopokewa MOI mwaka huo kuwa 10,944.
Wakati kuna hali hiyo, hivi karibuni hospitali hiyo ilibainisha kuwa nusu ya wagonjwa wanaofikishwa kwake kutokana na ajali, chanzo chake kinatokana na ajali za bodaboda.
Katika kipindi hicho, majeruhi 110,679 walipokewa MOI. Kati yao, waliotokana na ajali za bodaboda ni 59,671, magari 21,711 na ajali nyingine ni 29,297.
Alisema takwimu zinaonyesha waathiriwa wa ajali hizo ni pamoja na madereva, abiria na watembea kwa miguu.
Ngahyoma alifafanua kuwa asilimia 70 ya wagonjwa wanaopokewa MOI kutokana na ajali, hulazwa wodini, huku asilimia 10 hadi 15 wakifanyiwa uchunguzi.
Wakati MOI wakibainisha hayo, kuna taarifa njema kutoka Jeshi la Polisi ambalo kupitia kwa Kamishna wake wa Operesheni na Mafunzo, Makao Makuu, Lebaratus Sabas, linasema ajali za barabarani zimepungua kwa mwaka huu.
Sabas anabainisha kuwa, mwaka jana kulitokea ajali za barabarani 2,722 na kusababisha vifo 1,117 na majeruhi 2,717.
Kamanda Sabas anabainisha kuwa hadi Novemba mwaka huu, ajali zilikuwa 1,800 na waliofariki dunia ni 1,158 na majeruhi 2,089.