Taasisi ya Mifupa-MOI
Senior Member
- Apr 15, 2025
- 118
- 214
Taasisi ya Tiba ya Mifupa na Ubongo Muhimbili (MOI) imeendelea kung’ara katika utoaji wa huduma za matibabu ya mifupa katika ukanda wa nchi zinazoendelea na zinazopokea ufadhili wa vifaa tiba vya upasuaji wa mivunjiko ya mifupa kutoka shirika lisilo la kiserikali la nchini Marekani, Surgical Implant Generation Network (SIGN).
SIGN ni shirika ambalo kwa zaidi ya miaka 25 limekuwa likiratibu na kufadhili vipandikizi pamoja na vifaa vya upasuaji kwa nchi zinazoendelea, kwa lengo la kuboresha huduma za matibabu ya mifupa duniani.
Kupitia tathmini ya kimataifa iliyotolewa jana Januari 15, MOI imeshika nafasi ya pili kati ya hospitali 450 duniani kote zinazoshirikiana na SIGN.
Mafanikio hayo yameifanya MOI kuendelea kutambuliwa kama kituo cha umahiri wa tiba ya mifupa barani Afrika.
Akizungumza kuhusu mafanikio hayo, Mkurugenzi Mtendaji wa MOI, Mhe. Balozi Dkt. Mpoki Ulisubisya, amesema kuwa mafanikio hayo yametokana na umahiri, weledi na kujituma kwa madaktari bingwa na wabobezi wa MOI ambao wamekuwa wakihudumia wagonjwa kwa uzalendo mkubwa bila kuchoka.
Kwa upande wake, Daktari Bingwa wa Mifupa wa MOI, Dkt. William Mgisha, amesema kuwa kwa miaka mitatu mfululizo MOI imeendelea kushika nafasi ya pili duniani, ikitanguliwa na Hospitali ya Kossamaki iliyopo nchini Cambodia.
Dkt. Mgisha ameeleza kuwa umahiri huo umeiwezesha MOI kuendelea kupata ufadhili wa vifaa tiba vya SIGN Nail ambavyo vina gharama kubwa, na hivyo kusaidia wagonjwa wengi hususan majeruhi wa ajali za barabarani ambao wasingeweza kumudu gharama za matibabu hayo.
“Umahiri wa Taasisi yetu umechangia kwa kiasi kikubwa upatikanaji wa vifaa hivi muhimu vya tiba, ambavyo vimeokoa maisha na kurejesha matumaini kwa wagonjwa wengi,” amesema Dkt. Mgisha.
Katika juhudi za kuhakikisha huduma za kibingwa na kibobezi za mifupa zinawafikia wananchi wote, MOI imeendelea kuratibu huduma za tiba mkoba katika maeneo mbalimbali nchini, kuwajengea uwezo wataalam wa mifupa, pamoja na kufundisha madaktari bingwa wa mifupa ambao sasa wamesambaa katika mikoa mbalimbali nchini.