MOI yaendesha Mafunzo ya Kimataifa ya Saratani ya Mifupa na Misuli, Madaktari 200 wanashiriki

MOI yaendesha Mafunzo ya Kimataifa ya Saratani ya Mifupa na Misuli, Madaktari 200 wanashiriki

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Joined
Apr 18, 2017
Posts
3,984
Reaction score
13,760

Taasisi ya Tiba ya Mifupa Muhimbili (MOI) imezindua mafunzo ya kimataifa ya matibabu ya Saratani ya Mifupa na Misuli yanayofanyika kwa siku tatu ambapo zaidi ya madaktari 200 kutoka nchi mbalimbali ikiwemo Uingereza, Australia, Malaysia wanashiriki.
7029aaf5-91e1-4671-9042-28e289da0a33.jpg
Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa MOI, Dkt. Lemeri Mchome ameishukuru Serikali ya awamu ya sita kwa kuhakikisha huduma za kibingwa zinasogezwa nchini bila wagonjwa kulazimika kwenda nje ya nchi.
cc4626c3-ad5e-49d5-ba26-d25271d7cea9.jpg

f96eb948-4878-4ba5-b926-8930a3ae1855.jpg
“Mkutano huu wa kimataifa utaleta ufanisi wa kiwango cha kimataifa katika kutoa huduma hizi ,Pia utaharakisha utoaji wa huduma kwa wagonjwa na mwisho itawapunguzia wagonjwa usumbufu na gharama za kufuata huduma hizo nje ya nchi na kuokoa fedha za Serikali” Alisema Dkt. Mchome

Pia, Dkt. Mchome amemshukuru Mkurugenzi Mtendaji wa MOI, Prof. Abel Makubi kwa kuhakikisha mafunzo haya ya kimataifa yanafanyika hapa nchini ili kuwajengea uwezo wataalamu wa Tanzania na mataifa mengine barani Afrika na kuwa chachu ya utalii wa matibabu hapa nchini.



Upande wake Mkufunzi kutoka Chuo kikuu cha Oxford Uingereza, Prof. Duncan Whitwell amesema ni fahari kubwa kupata fursa ya kushiriki kwenye mafunzo hayo yenye lengo la kuboresha huduma kwa wagonjwa bila kulazimika kuzifuata huduma hizo nje ya nchi.

Naye, Daktari Bingwa wa Mifupa, Dkt. Violeth Lupondo amesema anajivunia kushiriki Mkutano wa kwanza wa Kitaifa wa Saratani ya Mifupa na Misuli Tanzania na mafunzo yatakuwa endelevu lengo ikiwa ni kuhakikisha huduma za kibingwa na bobezi zinapatikana MOI.
 
Yule mgonjwa aliyendeka wodini anaendeleaje?
 
Back
Top Bottom