Taasisi ya Mifupa-MOI
Senior Member
- Apr 15, 2025
- 118
- 214
Taasisi ya Tiba ya Mifupa na Ubongo Muhimbili (MOI) imeendelea kujiandaa kutoa huduma bora za kibingwa na kibobezi wakati wa Fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON) 2027, ambapo imeendesha mafunzo ya upasuaji wa magoti kwa njia ya matundu madogo kwa kushirikiana na wataalam kutoka Uingereza.
Akizungumza wakati wa ufunguzi wa mafunzo hayo leo Septemba 14, 2026, Mkurugenzi Mtendaji wa MOI, Mhe. Balozi Dkt. Mpoki Ulisubisya, amesema kuwa mafunzo hayo yatawajengea uwezo madaktari kufanya upasuaji wa magoti kwa njia ya matundu madogo (arthroscopy) kwa ufanisi zaidi.
“Mafunzo haya ni muendelezo wa jitihada za taasisi katika kuwekeza kwenye ujuzi ili kuboresha huduma…Tunatamani kufikia hatua ya kuwa na mtaala mmoja wa kufundishia kama ilivyo kwa marubani ambao hufundishwa kwa mtaala unaofanana duniani kote,” amesema Dkt. Mpoki.
Dkt. Mpoki amesema ushirikiano baina ya MOI na taasisi ya St. Roch Society ya Uingereza unawezesha kuimarisha utoaji wa tiba ya mifupa na majeraha kwa wanamichizo kuelekeza mashinadnao ya AFCON 2027, pamoja na wananchi wa kawaida.
Kwa upande wake, Dkt. Nic Bowman kutoka St. Roch Society ya Uingereza, ameushukuru uongozi wa MOI kwa mapokezi mazuri na ukarimu, akieleza kuwa ushirikiano kati ya taasisi hizo umeendelea kuimarika.
“MOI na St. Roch Society tumekuwa na mahusiano mazuri, na haya ni mafunzo yetu ya tatu tunayofanya kwa pamoja,” amesema Dkt. Bowmani.
Mafunzo hayo yamewakutanisha wataalam wa afya kutoka Tanzania, Ghana, Sudan Kusini, Kenya na Uganda, yakilenga kubadilishana uzoefu na kuongeza ujuzi katika teknolojia za kisasa za upasuaji wa magoti.
Ushirikiano huo unatarajiwa kuendelea kuimarisha uwezo wa wataalam wa ndani na kuongeza upatikanaji wa huduma za kibingwa za upasuaji wa magoti kwa njia ya matundu madogo nchini.