Taasisi ya Mifupa-MOI
Senior Member
- Apr 15, 2025
- 118
- 214
Taasisi ya Mifupa Muhimbili (MOI) imeendelea kuonesha dhamira yake ya kutoa huduma bora kwa wananchi kwa kuboresha mifumo ya utoaji huduma kwa viwango vya kimataifa na kuongeza uwajibikaji.
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dodoma kuhusu utekelezaji wa miradi ya maendeleo na fursa za vijana kwa mwaka 2025/2026, Mkurugenzi Mtendaji wa MOI, Mhe. Balozi Dkt. Mpoki Ulisubisya, amesema taasisi hiyo imefanikiwa kupunguza muda wa kusubiri huduma na kuongeza kiwango cha kuridhika kwa wateja kupitia maboresho ya kiteknolojia na mafunzo kwa watumishi.
“Naomba kutumia fursa hii kuwahakikishia wananchi wote na raia wa nchi zinazotuzunguka, hata mbali, kwamba tutaendelea kuwa kinara wa utoaji wa huduma bora kwa viwango vinavyokubalika kimataifa kwa wateja wote na kuwaondolea adha ya kutafuta huduma hizi nje ya bara la Afrika,” alisema Dkt. Ulisubisya.
Ameeleza kuwa katika mwaka wa fedha 2025/2026, MOI imeendelea kutekeleza agizo la Serikali la kusogeza huduma za kibingwa na kibobezi kwa wananchi kupitia huduma za tiba mkoba katika hospitali mbalimbali nchini. Hospitali hizo ni pamoja na Hospitali ya Nyangao (Lindi), Hospitali ya Mt. Benedict Ndanda (Mtwara), Hospitali ya Nkinga (Tabora), Hospitali ya Rufaa ya Kanda Chato (Geita), Hospitali ya Tosamaganga (Iringa), Hospitali ya Rufaa ya Mwalimu Nyerere (Musoma) na ALMC (Arusha).
Dkt. Ulisubisya, ameongeza kuwa katika kipindi cha mwaka 2025 pekee, MOI imehudumia jumla ya wagonjwa 180,000, ambapo kati yao wagonjwa 10,000 walipata huduma za kibobezi.
Aidha, amesema MOI kwa kushirikiana na Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili (MUHAS) imeendelea kufundisha wataalamu mabingwa wa mifupa, mishipa ya fahamu, upasuaji wa ubongo, usingizi na tiba ya ganzi akibainisha kuwa taasisi hiyo pia ni hospitali ya kufundishia vyuo vingine vikiwemo _College of Surgeons of East, Central and Southern Africa (COSECSA) na College of Anaesthesiologists of East, Central and Southern Africa (CANESCA).
Sambamba na hilo amesema MOI imeendelea kuwa na ushirikiano na hospitali na taasisi mbalimbali za ndani na nje ya nchi katika kujenga uwezo wa wataalamu kwenye maeneo ya tiba, utafiti na matumizi ya teknolojia mpya za kisasa.
Katika kupunguza msongamano wa wagonjwa, Dkt. Ulisubisya amesema huduma mpya za kibingwa na kibobezi zitaanzishwa na kusogezwa katika jengo la Upanga (zamani Tumaini) ili baadhi ya wagonjwa wa nje waanze kupata huduma huko, hatua itakayosaidia kupunguza msongamano katika makao makuu ya MOI.