MOI yashiriki maonyesho ya elimu ya juu Pemba, yatoa elimu kuhusu huduma za kibingwa na bobezi

MOI yashiriki maonyesho ya elimu ya juu Pemba, yatoa elimu kuhusu huduma za kibingwa na bobezi

Taasisi ya Mifupa-MOI

Senior Member
Joined
Apr 15, 2025
Posts
118
Reaction score
214
2e5c8048-3c1c-4e3d-b1ff-685760994a33.jpeg
Taasisi ya Tiba ya Mifupa na Ubongo Muhimbili MOI inashiriki kwa mara ya pili katika Maonesho ya Elimu ya Juu yanayofanyika viwanja vya Gombani, Pemba kwa lengo la kuwafahamisha wananchi juu ya huduma za kibingwa na kibobezi zinazopatikana nchini.

Ushiriki huo unalenga kupunguza idadi ya Watanzania wanaolazimika kusafiri nje ya nchi kutafuta matibabu ya mifupa, ubongo na mishipa ya fahamu kutokana na ukosefu wa taarifa.

Akizungumza katika banda la MOI leo Jumatano, Julai 23, 2026, Dkt. Zalina Shabhay, Daktari Bingwa wa Ubongo, Mgongo na Mishipa ya Fahamu wa MOI, amesema

"Tumeshiriki maonesho haya kutoa elimu. Kuna wananchi wengi wana changamoto za kiafya ambazo tungeweza kuzitibu MOI, lakini kwa sababu ya ukosefu wa taarifa wanaamua kukaa nyumbani au kutumia gharama kubwa kwenda nje ya nchi."

Dkt. Zalina amewataka wananchi wenye matatizo ya mifupa, ubongo na mishipa ya fahamu kufika MOI kwa ajili ya matibabu ya kibingwa na kibobezi.

Mmoja wa wakaazi wa Pemba, Saadi Omary, amesema ushiriki wa MOI umefungua macho kwa watu wengi visiwani humo. "Watu wengi hapa Pemba hatukujua huduma za mifupa na ubongo zinapatikana MOI. Sasa tumeelewa na tutawafikishia wenzetu habari hii," amesema Saadi.

MOI inapanua wigo wa Kutoa Elimu Nchi Nzima na hii ni mara ya pili kushiriki maonesho hayo. Mwaka 2025.

Uongozi wa MOI umesema utaendelea kushiriki katika mikoa mbalimbali nchini ili kuhakikisha huduma za kibingwa zinafika kwa kila Mtanzania.

Maonesho hayo yameanza leo Julai 23 na yatahitimishwa Julai 27, 2026.
 

Attachments

  • a878d836-0b54-45cc-bbdd-3beea80b7554.jpeg
    a878d836-0b54-45cc-bbdd-3beea80b7554.jpeg
    310.6 KB · Views: 12
Hamna huduma ya kunadirisha Ubongo wakuu ?

Kuna watu wana mambo ya ajabu sana, tunataka tujaribu wawekea hata ubongo wa kasuku labada wanaweza fanya mambo ya maana
 
Back
Top Bottom