MOI yashiriki Mkutano wa tatu wa PEN-PLUS kukabiliana na magonjwa yasiyoambukiza

MOI yashiriki Mkutano wa tatu wa PEN-PLUS kukabiliana na magonjwa yasiyoambukiza

Taasisi ya Mifupa-MOI

Senior Member
Joined
Apr 15, 2025
Posts
118
Reaction score
214
IMG-20260625-WA0003.jpg
Taasisi ya Tiba ya Mifupa na Ubongo Muhimbili (MOI) imeshiriki katika Mkutano wa 3 wa Kimataifa wa Kimkakati wa Kikanda wa PEN-PLUS unaolenga kujadili na kuimarisha mikakati ya kukabiliana na magonjwa yasiyoambukiza, unaofanyika katika Kituo cha Kimataifa cha Mikutano cha Julius Nyerere (JNICC) jijini Dar es Salaam.

Kupitia banda la Wizara ya Afya kitengo cha tiba utalii, MOI pamoja na Taasis nyingine za Afya, MOI imetoa elimu kwa washiriki wa mkutano kuhusu huduma mbalimbali za kibingwa na ubingwa bobezi zinazotolewa na taasisi hiyo katika matibabu ya kibobezi ya mifupa, ubongo, uti wa mgongo na mishipa ya fahamu.

Akizungumza wakati wa mkutano huo jana Jumatano Juni 23, 2026, Daktari Bingwa wa Upasuaji wa Ubongo MOI, Dkt. Zarina Shabhay, amesema ushiriki wa taasisi hiyo katika mkutano huo ni fursa muhimu ya kubadilishana uzoefu na wadau mbalimbali wa afya katika kuimarisha huduma za magonjwa yasiyoambukiza.
InShot_20260625_070526549.jpg

InShot_20260625_070555756.jpg
“Magonjwa yasiyoambukiza yanaendelea kuongezeka duniani, hivyo mikutano kama hii inatupa nafasi ya kujifunza, kushirikiana na kuweka mikakati madhubuti itakayosaidia kuboresha huduma za matibabu kwa wananchi,” amesema Dkt. Zarina

Mmoja wa washiriki waliotembelea banda la MOI, Bw. John George, amesema amefurahishwa na huduma na taarifa alizopata kutoka kwa wataalamu wa taasisi hiyo.

“Nimejifunza mambo mengi kuhusu huduma za kibingwa zinazotolewa MOI. Elimu niliyoipata itanisaidia mimi na familia yangu kutambua umuhimu wa kupata matibabu mapema na kutoka kwa wataalamu stahiki,” amesema Bw. John

Mkutano huo umezikutanisha nchi mbalimbali za Afrika pamoja na wadau wa sekta ya afya kwa lengo la kujadili njia bora za kuimarisha huduma za kinga, uchunguzi na matibabu ya magonjwa yasiyoambukiza katika ngazi zote za huduma za afya.
 
Back
Top Bottom