Moja kati ya changamoto za madaktari

Mung Chris

JF-Expert Member
Joined
Sep 12, 2017
Posts
3,391
Reaction score
3,849
Ma daktari wetu huku Africa huwa wanajitahidi sana kutuhudumia, wengine hujituma hadi kufanya tafiti ya tiba mbali mbali kwa maradhi mengine yanayoibuka kila leo, ila sasa wana changamoto moja tu.

Pale wanapoanza kuchukua vipimo vyote vinavyotakiwa kwa mgonjwa yakiwa magonjwa makubwa au madogo, tuache kuzungumzia uvimbe, vidonda ila magonjwa yale ambayo mgonjwa hujisikia kuumwa sana na daktari kuwa na muda mwingi wa kufikiria la kufanya.

Sasa changamoto inakuja pale ambapo pamoja na kuchukua vipimo vyote vinavyo hitajika ili kubaini tatizo la mgonjwa kisha kuishia kutopata majibu yani hamna ugonjwa au kila kitu kiko sawa au kila kiungo mwilini kiko sawa na hakuna tatizo au mwilini hana tatizo lolote lile, ila mgonjwa analia au anajiskia kuumwa sana.

Vipimo vyote vinaonyesha hamna shida. Hii ni changamoto kubwa kwa madaktari wetu wanakutana nayo na hili madactari huwa wana tatuaje.
 
Africa bado hatuna advanced technology, vipimo kama colonoscopy, endoscopy, vinaweza kugundua matatizo yaliyojificha zaidi kama cancer. Au MRI na CT scan.
Kwa kifupi bado tunaishi kwa kudra za Mwenyezi Mungu
 
Africa bado hatuna advanced technology, vipimo kama colonoscopy, endoscopy, vinaweza kugundua matatizo yaliyojificha zaidi kama cancer. Au MRI na CT scan.
Kwa kifupi bado tunaishi kwa kudra za Mwenyezi Mungu
Sky Eclat nazungumzia vipimo vyote hivyo vya colonoscopy, endoscopy, MRI na CT scan havioni chochote hapo wanafanyaje.
 
I Think Ni kustep Down Problems to Herbalist Or Step Up To invisible Power
 
Hata blood culture hakuna kitu. inaelekea ww ni Nurse/ daktari au medical practitioner sasa Sky Eclat inakuwaje hapa wanafanyaje.
Umeamua kumwambia muda gani na unaumwa sehemu gani ya mwili? Ukipima maumivu yako katika scale ya 0-10 unaweza kuyapa namba ngapi?
 
Umeamua kumwambia muda gani na unaumwa sehemu gani ya mwili? Ukipima maumivu yako katika scale ya 0-10 unaweza kuyapa namba ngapi?
hata ukipima katika scale ya 0-10 ndio utajua aina ya ugonjwa?
 
Siyo kila maumivu yanaashiria infection mkuu,mengine ni psychological tu. Sasa mtu Kama ameachwa au kufumania na hayuko katika nafasi ya kuweka hilo hadharani unadhani kipimo gani kitakuwa positive hapo[emoji135]Jenga imani na mgonjwa,tuliza maumivu,mthibitishie faragha halafu anza upya[emoji3]lazima afunguke tu.
 
Naombeni mnieleweshe.
1.Inakuwaje unampeleka mgonjwa hospitali A anapimwa unaambiwa haumwi,unampeleka hospitali B unaambiwa anaumwa.
2. Kwa nini hospitali za kibongo wanashindwa kugundua ugonjwa wa kansa katika hatua za awali. Mpaka imekolea au mgonjwa yuko hoi ndo wanakuja kusema inawezekana ni kansa.
 
Me nafikiri kutotambua mgonjwa anaumwa nn kwanza huwenda mgonjwa historia anayotoa haijajitosheleza
 
Kidogo nimekuelewa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…