Robert Heriel Mtibeli
JF-Expert Member
- Mar 24, 2018
- 28,297
- 68,017
Mpo salama Kabisa!
Ukiona watoto au kijana ambaye ni fuata mkumbo, fasheni, mfuasi na kawageuza Wasanii wa Muziki, Drama, na Filamu kuwa Role model ujue tayari mzazi au mlezi kuna mahali amefeli.
Na ili umfelishe mtu yeyote au Jamii yeyote itakupasa uwape nguvu Wasanii wa drama, Filamu na Muziki. Ndio Njia rahisi Kabisa ya kumfelisha Mtu hasa Akiwa mchanga Kabisa, kijana.
Jamii Makini na ambazo zinaweza WA kufanya mabadiliko makubwa kwa wakati hujao hudhibiti Sana Masuala ya Filamu, Muziki na drama. Huyapa kipombele kidogo na kuyadhibiti yasionekane kirahisi kwa Watoto na vijana wadogo.
Ni kupitia Muziki, drama na Filamu ndipo mtoto anaweza kuharibiwa vibaya future yake, mitazamo yake, uwezo wake wa kufikiri na mitindo yake ya Maisha.
Wazazi wenye mipango ya kutawala wengine, wazazi wenye kuandaa watoto kuwa success Planner, huwadhibiti watoto kuangalia mambo ya hovyo mtandaoni na kwenye Luninga.
Mtoto wa Miaka chini ya kumi na nane. Hatoweza Kupata faida yoyote Ile kwa kuangalia na kusikiliza Muziki wa kisasa, drama na Filamu za kisasa zilizojaa Maudhui yaliyokosa maadili.
Vijana wengi wa Miaka ya 80-90 walioharibika kwa kutumia madawa ya kulevya, kujiingiza kwenye ushoga na usagaji, kutembea uchi , kujichora Tattoo wengi wao ni matokeo ya kuwaiga Wasanii wa Muziki, drama na Filamu.
Mimi ni Mtunzi wa Simulizi pamoja na scene za drama na Filamu. Kama Mtunzi ambaye zipo baadhi ya scene nilizozitunga kwa baadhi ya Filamu na tamthilia. Ninafahamu Kile ninachokisema kutokana na Kazi za utunzi, uongozaji na utayarishaji wa Filamu.
Haiwi bahati mbaya Wasanii kukaa uchi. Haiwi bahati mbaya kwenye Filamu kuonyesha urahisi katika maisha, na wahusika kukaa uchi. Sio kwa bahati Mbaya..
Unafikiri haiwezekani Wasanii wa Muziki, drama au Filamu kuigiza Bila uchafu na mambo yasiyofaa. Inawezekana Kabisa.
Ni jukumu la mzazi kudhibiti mtoto wake mwenye umri chini ya miaka 18 anayemtegemea na ambaye yupo nyumbani kuangalia Muziki wa kisasa, drama na Filamu.
Mtoto aliyeanza kujitegemea, uliyemfunza akafunzika ndiye anaweza kuanza kuangalia hao wasanii kwani tayari ushamjenga na hawezi kuhadaika na Drama, ulaghai na propaganda mbaya zinazoendeshwa nao.
Watoto wadogo hawapaswi kuyachukulia maisha kama Entertainment na Sports. Kwani maisha sio burudani na michezo.
Maisha ni KAZI kwa asilimia tisini
Kisha burudani na Michezo ndio kwa asilimia 10.
Mtoto mdogo kuanza kuchukulia maisha ni burudani na Michezo ni kumfanya aendekeze Michezo na burudani kwa asilimia 90% na Kazi asilimia 10.
Ahsante Sana.
Mtibeli, Safarini