Moja ya Dalili ya Kiongozi Mpumbavu ni kutaka kuogopwa.

Moja ya Dalili ya Kiongozi Mpumbavu ni kutaka kuogopwa.

Robert Heriel Mtibeli

JF-Expert Member
Joined
Mar 24, 2018
Posts
28,297
Reaction score
68,017
Wakuu Kwema!

Leo sina mengi Sana ya kusema,
Mtoto wangu aliniuliza hivi; Baba ni Dalili gani ya wazi itakayonifanya nimjue kiongozi huyu ni Mpumbavu ili nijiepushe naye?

Swali lake linashangaza Sana. Ukizingatia yeye ni mtoto wa miaka sita tuu.

Nikamjibu;
Kiongozi Mpumbavu utamtambua Kwa dalili ya yeye kutaka kuogopwa.
Alafu Dalili ya pili, inafanana na hiyo ya Kwanza, ambayo; KUDHANI ANAOGOPEKA.

Hivyo ndivyo nilivyomjibu mwanangu,
Akanishukuru Sana alafu akasema; Sawa nitaweza kujiepusha.na kiongozi Mpumbavu.

Nilitaka kumuuliza atajiepusha naye wapi, nikafikiri isijekuwa ananisema kidizaini Baba yake,

Anyways, niseme tuu. Ukijiona unadhani kwenye akili yako watu wanakuogopa jua tayari upo kwenye kundi la watu wapumbavu, lakini ukiwa unafanya juhudi watu wakuogope basi wewe upo Kwenye Upumbavu Mkuu.

SABATO NJEMA.
 
Kuna kiongozi mmoja lilikuwa linapenda kuogopwa mpaka wakaliita Mungu, Yeah nk. Povu ruksa
 
Kuna quote niliiona humu jf kuna member aliiandika inasema.
Uikiona mtu ameshindwa kukuheshimu basi hakikisha anakuogopa.

Maishani hakuna watu wanaoheshimu wengine unless uwe unawaobey wao, sasa huo ni ujinga.
Hivyo hakikisha wanakaa mbali na wewe au wakuogope.

Au siku zote utakuwa mjinga anayetumika na dustbin la machafu ya wengine.
So no, sio upumbavu bali ni way of life heshimu uheshimiwe au hakuna amani, unachotoa ndicho unachopata.
 
Back
Top Bottom