Moja ya hatua unazoweza kufuata kwenye kujiandaa kuacha kazi na kujiajiri

CHASHA FARMING

JF-Expert Member
Joined
Jun 4, 2011
Posts
7,872
Reaction score
9,263
Habari za mida wakuu?

Kwanza ifahamike kwamba kuacha kazi na kuingia kwenye ajira binafisi ni zoezi gumu sana. ni maamuzi magumu na huenda ndo maamuzi magumu kabisa ni zaidi ya maamuzi ya kupeana talaka.



Katika watu 1000 ni watu watatu tu wanao weza kuchukua huo uamuzi mugumu kabisa.

Hii ni kutokana na ukweli kwamba unakuta tiyari mentality iko kwenye kuajiriwa.

SASA TUNAFANYAJE?.AU TUNAKOMAA NA KAZI?

1.Anza kwa kubadili marafiki, na watu wengine wanao kuzunguka. Marafiki ambao unaona malengo yao ni miselei unatakiwa kuanza kuwa kwepa sana na anza kuambata na wale walio kwenye ajira binafisi. hawa mkikutana story zitakuwa ni za Biashara tu.

2. Jitahidi sana kuishi maisha normal, hii ni kwa muda wote, ishi levo ya kawaida ila mahitaji yote yawepo.Familia yako izoeshe hayo maisha normal.

3. Kama una mke/mme hakikisha anakuwa bise asikae tu, usiplani kuacha kazi ilihali mke ni Golikipa, hakikisha anaingiza chochote kile hata kama ni Tsh 3000 kwa siku.

3. Watoto wako, kama wako wakubwa kabisa 18+basi wasikae nyumbani na kula na wao wapangie majukumu yaani ilimuradi kila mmoja awe na mchango fulani, wanaweza kuwa wafanyakazi kwenye project yako mpya au basi wafungulie vimradi vyao n waambie hapo ndo pesa yao ya kula, na kuvaa itakapo toka.

4. Ndugu na jamaa anza kuwapa live kuhusu misaada na bakiza misaada muhimu pekeee, kama matibabu au Ugonjwa.

Kama ndugu zako wana nguvu wafanye kazi na kama vipi chukua waje kukusaidia wawe sehemu ya wafanya kazi.

Hata wazazi kama wana nguvu bado za kutosha wasisitize wafanye kazi pia.

5. Kama una pesa ya kutosha kata kabisa bima ya afya ya familia yako yote. Hakuna kitu kina kula pesa kama matibabu yaani unaweza filisika au mtaji unaweza ishia kwenye kuuguza.

6. Kama umepanga pia lipa hata kodi ya mwaka mzima.

7. Kazini anza kuwaza kazi zako muda wote na ukiwa kazini ukaanza kusikia wana mjadala wa masilahi ya wafanya kazi wewe kula kona, omba hata uzuru na ondoka.

8.Kama una Idea yako tiyari basi anzisha project yako ila hii iwe ni dakika zako za mwisho kabisa kazini.

Nitaelezea kwa nini iwe ni dakika za mwisho ndo uanzishe mradi na isiwe kabla sana.

9.Wakati wa likizo au weekend fanya ziara nyingi sana za kuwatembelea walio jiajiri, hasa wanao fanya kile unacho taka kufanya wewe, achana kabisa na viwanja kwa muda huo.

10.Andaa plan yako sasa hasa ya maisha ya ulaiani.
- Familia itaishi vipi,
-Itakula vipi
-Itavaa vipi,
-Ada za wa toto na kadhalila.

Hapa sasa tumia ile ya kule juu kwamba mke awe bise sana na na mnaweza panga kwamba pesa au faida ya biashara fulani itakuwa ni kwa ajili ya Chakula cha nyumbani na pia ada na mavazi.

Na biashara fulani ni.kwa ajili ya Ada ya shule pekee,
Ndo.maana nikasisitiza mama au mzee atangulie fild hata mwaka 1 kabla.

11. Hakikisha usha plan project yako na usha soma kila kitu na inavyo endeswa na hatari zake.

Kamwe usiache ndo ufike home uanze kuuliza watu ufanye nini, hakikisha unafanya utafiti wa kutosha na wa kitalaamu.

Kamwe usifanye kwa sababu jamaa zako au ndugu anafanya au umeshauriwa, no fanya utafiti wa kutosha

13. Hapa sasa unaweza toa notce ya mwezi, waambie ukweli ingawa hapa sasa unaweza kutana na vikwazo vya kutosha kutoka kwa wafanya kazi hasa bosi wako ila kwa sababu usha amua basi wewe aga na waambie ni.maamuzi yako.

14 Hand over kila kitu na kuka kona kama watakufanyia part poa tu.

15.Sasa usha ingia kitaaa, hakikisha kesho yake tiyari uko bise yaani usiache then ukajipa muda wa kupumzika na sijui kwenda kusalimia.

Kuwa bise kadri iwezekanavyo.

NB: Kuacha kazi ni maamuzi magumu sana na yanapaswa kuandkkwa kwenye story ya mafanikio yako.

Mimi sijatumia baadhi ya njia ingawa kuna baadhi hapo jiu nilizitumia.

UJASIRIAMALI SIO.LELE MAMA KUNA WAKATI UTAKUWA UNAONGEA HATA MWENYEWE NJIANI.

MUHIMU
Unapo taka kuacha kazi kamwe na daima usianze kutafuta ushauri kwa watu walioko kwenye ajira, kama ni ushauri basi tafuta kwa watu walio nje ya ajira yaani walio jiajiri wenyewe.


MWISHO
Humu hakuna mtoto hivyo hakuna anaye Danganywa kila mtu na maamuzi yake, ieleweke hivyo.

Chasha Poultry Farm
 
Ahsante mkuu ujumbe mzuri.
 
Kweli kaka imekaa Poa sanaa kwa kweli Uhuru ni kitu kizuriiii sanaa...
 
Mkuu umeongea facts kabisa anayetaka kujiajiri au kuwa na kibiashara chake inabidi ajiandae kisaikolojia pia ajue kuna vitu atavikosa kabisa

Na stress ni nyingi ila kwa kauli tunasema there is no perfect time just excute..... eat shit 12 month then eat well the rest of your life
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…