Moja ya jambo bora kufanywa na Magufuli ni kuanzisha kiwanda cha sukari Bagamoyo

Moja ya jambo bora kufanywa na Magufuli ni kuanzisha kiwanda cha sukari Bagamoyo

Red Giant

JF-Expert Member
Joined
Mar 9, 2012
Posts
15,657
Reaction score
20,967
Magufuli alimpatia mzee Bakhresa ekari karibia Elfu ishirini huko Bagamoyo ili alime miwa na kuzalisha sukari. Jamaa kafanya kweli. Inakadiriwa kuwa nchi yetu mahitaji ya sukari kwa mwaka ni tani 700,000 lakini uzalishaji ni kama tani 400,000. kiwanda cha Bakhresa kinategemewa kuzalisha tani 30,000. Safari ya kuweza kujitosheleza bado ndefu sana.

Sababu nchi yetu ni kubwa na ina mabonde kibao mito na maziwa, wawekezaji wengine wengi; hasa wa ndani, wangepewa maeneo zaidi wazalishe sukari. Ni aibu kwa linchi kama Tanzania kushindwa kuzalisha sukari ya kutosha wakati Mauritius ambayo inaingia kwa Tanzania karibu mara 500, wanazalisha tani 500,000 kwa mwaka.

Magufuli atakumbukwa kwa jambo hili zuri alilofanya. Kiwanda hicho kitazalisha ajira za kutosha kiwandani na outgrowers kibao ambao wametengewa karibia ekari 7,000

Kuna wawekezaji wanaotaka maeneo ya kulima miwa Tanzania wamenyimwa hayo maeneo?
 
Kwa nini unasema Magufuli ndiye alianzisha kiwanda cha sukari Bagamoyo na sio Bakhresa?
kwenye video ya kwanza anaonekana Magufuli akimwambia mzee Bakhresa kuwa ampatie shamba Bagamoyo alime miwa. Inaonekana upembuzi yakinifu hapo ulifanywa muda mrefu sana, hakupatikana tu mtu.
 
Kwa nini unafikiri nj lazima au muhimu sana nchi izalishe yenyewe ndani sukari ya kujitosheleza?
 
Kuna wawekezaji wanaotaka maeneo ya kulima miwa Tanzania wamenyimwa hayo maeneo?
Sometimes serikali ndiyo inatakiwa kuanzisha. Itafute watu, iwaonyeshe maeneo na kuwapa incentives, hata kwa mikopo au kuwadhamini kwenye taasisi za pesa nk.

Kama hapa inaonekana kama Bakhresa hakuwa na mpango huo ila Magufuli akalianzisha.
 
Magufuli alikuwa na mashamba makubwa kiasi hicho cha kuweza kuwapatia wawekezaji?

Hata kama hayo mashamba yalikuwa ni yake ina maana kwamba Kiwanda pia yeye ndiye aliyekianzisha?

Wewe ukimpa mtu eneo lako ajenge nyumba ina maana wewe ndiye umejenga hiyo nyumba?

kwenye video ya kwanza anaonekana Magufuli akimwambia mzee Bakhresa kuwa ampatie shamba Bagamoyo alime miwa. Inaonekana upembuzi yakinifu hapo ulifanywa muda mrefu sana, hakupatikana tu mtu.
 
Tutafika tuuu ila kwa ccm hii nchi ya ahadi itatuchukua miaka 300,000 kuifikia...
Stupid kantre...
 
Kwa nini unafikiri nj lazima au muhimu sana nchi izalishe yenyewe ndani sukari ya kujitosheleza?
Faida nyingi mkuu. Ajira, pesa za kigeni tukiexport nk.
 
Kwa nini unasema Magufuli ndiye alianzisha kiwanda cha sukari Bagamoyo na sio Bakhresa?
Ye ndio alimshawishi bakhresa ajenge kiwanda cha sukari na alimuahidi kumpa hilo eneo.

Kwa hii idea bakhresa hatomsahau magufuli. Maana unaweza kuwa na pesa na usiwe na idea ya kufanya jambo la msingi.

Nadhani ukitoa juisi, ice cream, biskuti, lambalamba, hotel, boti ziendazo kasi..kiwanda cha sukari kinaweza kuwa moja ya mradi mkubwa sana na wa uhakika wa bakhresa ambao bado ushindani ni mdogo ukilinganisha na hizo bidhaa nyingine.
 
Magufuli alikuwa na mashamba makubwa kiasi hicho cha kuweza kuwapatia wawekezaji ?
Hata kama hayo mashamba yalikuwa ni yake ina maana kwamba Kiwanda pia yeye ndiye aliyekianzisha?
Wewe ukimpa mtu eneo lako ajenge nyumba ina maana wewe ndiye umejenga hiyo nyumba?
Unaweza anzisha kitu kwa kutoa idea tu.
 
Kwa taarifa yako madini tume kuwa tuna export tangu tupate uhuru.

Halafu kwa nini unafikiria ku export kabla ya kushusha bei ya sukari inayopanda kila kukicha?
Faida nyingi mkuu. Ajira, pesa za kigeni tukiexport nk.
 
Back
Top Bottom