Moja ya jambo bora kufanywa na Magufuli ni kuanzisha kiwanda cha sukari Bagamoyo

Kwa nini unafikiri nj lazima au muhimu sana nchi izalishe yenyewe ndani sukari ya kujitosheleza?
Kutoa ajira, kuondoa urasimu kwenye soko la sukari, uhakika na usalama kwa watumiaji maana enzi za jk ilikuwa inakuja sukari reject au iliyo expire kutoka brazil. Mara nyingi ulikuwa ukifika madukani unaona nyuki wamezunguka beseni la sukari au nyingine ukitia kwenye chai unaona kama kuna vichupa chupa vinaelea. Tumekula sana sumu.
 
Unafikiri baada ya miaka 3 ijayo mahitaji yetu ya sukari bado yataendelea kuwa tana laki 7?
 
Kwa taarifa yako madini tume kuwa tuna export tangu tupate uhuru.

Halafu kwa nini unafikiria ku export kabla ya kushusha bei ya sukari inayopanda kila kukicha?
Huko nako Magufuli alifanya vitu vizuri sana. Tulikuwa tunaexport kwa kulanguliwa, jamaa akanzisha masoko ya dhahabu/madini. Serikali ikaanza kupata pesa ya maana, wachimbaji bei nzuri nk. Cheki miji ya wachimbaji kama Geita na Chunya ilivyobadilika ndani ya muda mfupi. Haya maswala ni mipango tu, bila mipango mnaweza export madini miak elfu na kubaki maskini.

Hiyo ya kushusha bei nayo ni faida pia, japo itachukua muda mpaka pale tutakapoweza kujitosheleza katika uzalishaji wa ndani.
 
Hiyo pesa ya maana serikali iliyokuwa inapata ilikuwa inaenda wapi?
 
Usikariri kujitosheleza uzalishaji wa ndani, hayo ni maneno ya wanasiasa tu.
Mataifa mengi tajiri kuanzia Japan, Singapore, ya ulaya, uarabuni wala hayajitoshelezi uzalishaji wa ndani na raia wake wana maisha bora kuliko sehemu kubwa ya dunia.
 
Waliporwa wawekezaji wanaitwa Eco Energy.ndo wenye eneo lao toka enzi Raisi ni Mwinyi.Hii itakuja kiwa Case kama ile ya Kaburu Stein aliwai shikiria Ndege SA https://www.ippmedia.com/en/news/bagamoyo-ecoenergy-takes-govt-arbitration
Limekaa vibaya, natumaini litaisha salama. Japo hizi kampuni nyingine zinakuwaga za mfukoni, madalali tu wanaohodhi eneo na kuanza kutafuta mitaji. Nimesoma hiyo article kwamba jamaa walipewa hekta 20,000. Bakhresa kamegewa kama 8,000. Wakubaliane wapewe waendeleze zilizobaki.
 
JPM mzee wa kuacha ALAMA KUBWA KUBWA....

JPM mzee wa MAAMUZI MAKUBWA NA MAZITO.....

Hakika LEGACY yake ipo ,itakuwepo na itaishi.....

Barukh Atah Adonai Eloheinu melekh ha'olam dayan ha-emet 🤲🤲

Yetzer Ha-Tov

RiP JPM ,amen 🤲

#SiempreSSH
#SiempreJMT
#NchiKwanza
 
"Sababu nchi yetu ni kubwa na ina mabonde kibao mito na maziwa, wawekezaji wengine wengi; hasa wa ndani, wangepewa maeneo zaidi wazalishe sukari"
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…