Lycaon pictus
JF-Expert Member
- Jan 31, 2021
- 11,884
- 21,175
Huwezi kamwe kuwa kiongozi bora kama hufahamu na huelewi takwimu. Yaani kujua zinamaanisha nini. Takwimu ndiyo zinakuambia ulipo, ulipotoka na unatakiwa uende wapi na kwa namna gani. Takwimu zinakupa picha ambayo ni clear kabisa.
Ukimsoma Nyerere unaona alitumia sana Takwimu na alizielewa vyema zinachomaanisha. Mara nyingi utamsoma akitumia percent. Akisema labda ishirini kwa mia, 40 kwa mia, mbili kwa mia nk nk.
Tokea enzi anadai uhuru alikuwa mtu wa kujenga hoja zake kwa takwimu, siyo maneno matupu matupu tu. Kwenye kijitabu kilio cha uhuru.
Anaeleza kitakwimu jinsi weupe wachache(Wazungu na Waasia) walivyopendelewa, huku Waafrika wengi wakikandamizwa kwenye uchumi, elimu na siasa.
Kwenye kijitabu Uhuru mpaka Jamhuri anaeleza vema kitakwimu juu ya mafanikio ya mwaka mmoja wa uhuru, na kwa nini kimahesabu ilikuwa sawa kung'oa reli ya Mtwara.
Kwenye kitabu Tanzania itajengwa na wenye moyo aliyotoa baada ya kuwafukuza wanachuo waliokataa kwenda JKT. Kaweka data humo ndani hadi mtu unayemsoma unasema hawa wanafunzi namna gani!!
Mtu yeyote akitaka kuwa kiongozi bora, wa kitu chochote, anapaswa kumuiga Nyerere katika kufahamu takwimu na kuzielewa vema.
Kwenye kitabu elimu ya kujitegemea aligundua kuwa kiasi kikubwa sana cha wanafunzi hawaendi sekondari. Akaja na sera kwamba elimu inayotolewa iwasaidie hawa wengi ambao hawaendi sekondari. Pia ndiyo akaja na sera ya kuanza la kwanza na miaka 7 badala ya mitano. Lengo ni kuwa huyu anayemaliza darasa la saba awe walau na umri wa kumuwezesha kufanya shughuli za kujitegemeza.