NDUKI
JF-Expert Member
- Jan 19, 2013
- 3,422
- 2,418
Habari zenu.
Natumai mpo salama kabisa, nimeona nominees wa Tuzo za Muziki Tanzania kiukweli watu wengi wametilia mashaka jinsi walivyopatikana hao washindani.
Hili jambo natumai kwa asilimia kubwa kabisa lina baraka zote kutoka kwa Baraza la Sanaa Tanzania mpaka ikafikiwa kutangazwa kwa jamii ili kupatikana kwa washindi.
Niliona humu jamvini watu wakilalamika kuhusu nominees waliowekwa kwenye kundi la MWANAHIP HOP Bora wa mwaka kuwa hawakustahili, kwa sababu gani, wanazo sababu walizozitaja kwenye thread inayozungumzia Tuzo hizo.
Lakini pia nimekutana na kituko kingine cha Msanii Conboy kuwekwa nominee akiwa na Album ya Street Ties. Kiuhalisia hiyo sio Album na hata Conboy mwenyewe aliiita hiyo ni EP inakuaje kwenye hizi Tuzo iwekwe kwenye kundi la Album?
View attachment 2585432
Nashindwa kuelewa kabisa tatizo liko wapi. Natumai kuna shida mahali, kama kumbukumbu yangu inavyonikumbusha mwaka jana au juzi kulitokea tena kituko kama si vituko, walimuweka Damian Soul na wimbo wake wa Amsha Mapopo akiwa kama ni Msanii Chipukizi wakati yupo miaka mingi tu kwenye game.
Linalotia ukakasi zaidi, tunae Naibu Waziri ambaye pia ni mdau KINDAKINDAKI na anaujua vizuri sana huu muziki na pia ni kiongozi kama sikosei wa Tanzania Urban Music Association (TUMA) inakuaje kunakuwa na makosa kama haya? Natumai wakuu wengi wanapitia humu, hivyo wataliona hili na kulifanyia kazi.
Nawasilisha.