Mojawapo wa matapeli wa magari bandarini hawa hapa

IPILIMO

JF-Expert Member
Joined
Oct 13, 2012
Posts
1,819
Reaction score
801
hata wewe unayedhani huwezi tapeliwa be warned; matapeli wako wengi sana, na sio lazima uwe unataka cha urahisi, bali kuna wakati inatokea katika situation ya kawaida tu maishani.
 
Duh pole kwa kuingizwa mkenge, tafadhali toa taarifa Polisi au fungua Kesi wao wanajua wata wa charge kwa kosa gani. Lakini pia nina amini Polisi kwa kushirikiana na wamiliki wa mitandao ya simu wanaweza kufanikisha kuwakamta hao WASHENZI. Pia hapo Bandarini kuna sehemu wana CCCTV Camera kama wanaweza kuangalia ili waweze kutoa japo picha na kuzisambaza kwa umaa
 
duh pole kwa kuingizwa mkenge, tafadhali toa taarifa polisi au fungua kesi wao wanajua wata wa charge kwa kosa gani. Lakini pia nina amini polisi kwa kushirikiana na wamiliki wa mitandao ya simu wanaweza kufanikisha kuwakamta hao washenzi. Pia hapo bandarini kuna sehemu wana ccctv camera kama wanaweza kuangalia ili waweze kutoa japo picha na kuzisambaza kwa umaa

nashukuru mkuu kwa ushauri wako! Nina majina yao tu na namba zao. Sijui wanaishi wapi exactly japo ni dsm. Je kama walikuwa wanatumia namba za simu feki (za muda tu) kisha wametupa, au walisajili kwa majina tofauti maana kuna matatizo sana katika usajili (wengine wanasajilisha hata bila kitambulisho....wanasema mteja apeleke kitambulisho baada ya kusajiriwa).
Nitaomba unisaidie zaidi hatua zinginezo kama unafahamu ili mradi niwapate.
 
INAUMA KUTAPELIWA, NA SIKU YA KUTAPELIWA HUJA KAMA AJALI; NA AJALI HAINA MWENYEWE!! waliomtapeli mdogo wangu, bandarini kwa kuwaihidi kumfanyia mpango wa Gari za Mnada bandarini (zisizo lipwa ushuru) kwakweli dogo aliingia hadi bandarini, akakagua gari, akaambiwa alipe kisha process alizoambiwa ziendelee, yeye asubiri, akasubiri masaa aliyoambiwa...... hadi leo jamaa alipotelea palepale bandarini hakuonekana, simu haipatikani hadi leo!!! namba za matepeli hao ni 0653147021 -huyu ni mdada anaitwa Halima, 0784929778-huyu mwanaume ndo kiunganishi (atakwambia kuhusu kupata gari bandarini ilivo rahisi, na atakuaminisha hadi unaingia laini kama ndio mara yako ya kwanza kusikia hili) na kisha huyu mwanaume anaitwa Shomari Mhunzi- 0753162892 (kwa mjibu wa usajiri wa vodacom)- ndio anakupeleka bandarini ndani hadi kukagua gari-kisha anakupa process--unalipia, kisha anasema subiri sehemu amalize akuletee listi kisha process za kulipa zifuate.
Hao matapeli sijui kama wana ID humu JF, ila hutembelea humu, hasa kwenye thread ya wanaotaka magari humu; ndipo yeye hutafuta mawasiliano na kukupigia.

NAOMBA kama kuna aliye athirika na hawa, hata kama bado wanawasiliana hawajafikia hatua ya kufanya biashara husika, itambulike hivyo kuhusu watu hawa, tusaidiane kuwapata kwa wenye weledi huo. NA inawezekana wanapitia UZI huu, Nawaambia Ni kweli kwa Binadamu inaweza kuwa haiwezekani kuwapata kirahisi; Ila kwa Mungu inawezekana, maana hata sasa YEYE anawaona walipo, wanachofanya na hata wana waza nini, Pia Mungu si dhalimu kiasi cha kufanya wengine walie kwa ajili ya utapeli huo na wao wakabaki wanakula BATA tu kwa hela ya maskini (bora ingekuwa ya kifisadi). Muiomba Mungu hujibiwa, haijalishi lini, lakini Mungu anajua na hapendi udhalimu wa aina hii na unaofanana. WARUDISHE PESA ZA WATU. Matapeli jiangalieni, wengine hawatamtegemea Mungu, Ila duniani kuna Miungu HATARI kuliko rehema za Mungu!! watch out!!!

Naomba ushirikiano wenu, na wengine pia msiingie mkenge kwa utapeli wa namna hii: (be warned)

Mi nataka waje nitapeli mm nionyeshe mfano. Wataacha hyo michezo siku hyo hyo. Sipeleki mtu polisi.
 
Mkuu pole sana, Nchi hii imeoza kila sehemu.
 
wanakula pamoja na washkaji wa TRA na wa TPA.kwaiyo ni ngumu kuwashika bila msaada wa TRA na TPA.
 
hawa lazma wanakula na watumishi TRA na TPA kufanikisha maovu yao cha msingi washajulikana ni kuwa makini na tisipende miteremko jamani ina gharama
 
karibu jijini!!!! unafikiri gari ni bajaji uchukue kwa masaa tu liwe lako
 
hapo makosa pia yako kwa aliyetapeliwa. toka lini watu "wakafanyiwa mpango...." bandarini? Acheni tamaa za ki.p.umbavu! Agiza gari, nunua toka yadi au subiri mnada wa hadhara. Ukitaka short-cut na upigwe tu! Ungelinunua kwa "kufanyiwa mpango" maana yake ungekwepa kodi yetu. halafu nyie ndio mmejaa JF kutoa mapovu ya eskro kumbe na nyie ni misingiseti huko mitaani!
Halafu bila aibu unamhusisha Mungu, Mungu yupi huyo wa boko haram? yani ulitaka mungu awasaidie kupiga gari la dili?
 
Duh pole kwa kuingizwa mkenge, tafadhali toa taarifa Polisi au fungua Kesi wao wanajua wata wa charge kwa kosa gani. Lakini pia nina amini Polisi kwa kushirikiana na wamiliki wa mitandao ya simu wanaweza kufanikisha kuwakamta hao WASHENZI. Pia hapo Bandarini kuna sehemu wana CCCTV Camera kama wanaweza kuangalia ili waweze kutoa japo picha na kuzisambaza kwa umaa

akienda polisi na yeye atakamatwa, huwezi kwenda kulalamika kwa kutapeliwa katika dili ya kihalifu! Yani polisi wawakamate watu waliokutapeli kwa kutokuuzia gari kinyume na sheria?
 
INAUMA KUTAPELIWA, NA SIKU YA KUTAPELIWA HUJA KAMA AJALI; NA AJALI HAINA MWENYEWE!! waliomtapeli mdogo wangu, bandarini kwa kuwaihidi kumfanyia mpango wa Gari za Mnada bandarini (zisizo lipwa ushuru) kwakweli dogo aliingia hadi bandarini, akakagua gari, akaambiwa alipe kisha process alizoambiwa ziendelee, yeye asubiri, akasubiri masaa aliyoambiwa...... hadi leo jamaa alipotelea palepale bandarini hakuonekana, simu haipatikani hadi leo!!! namba za matepeli hao ni 0653147021 -huyu ni mdada anaitwa Halima, 0784929778-huyu mwanaume ndo kiunganishi (atakwambia kuhusu kupata gari bandarini ilivo rahisi, na atakuaminisha hadi unaingia laini kama ndio mara yako ya kwanza kusikia hili) na kisha huyu mwanaume anaitwa Shomari Mhunzi- 0753162892 (kwa mjibu wa usajiri wa vodacom)- ndio anakupeleka bandarini ndani hadi kukagua gari-kisha anakupa process--unalipia, kisha anasema subiri sehemu amalize akuletee listi kisha process za kulipa zifuate.
Hao matapeli sijui kama wana ID humu JF, ila hutembelea humu, hasa kwenye thread ya wanaotaka magari humu; ndipo yeye hutafuta mawasiliano na kukupigia.

NAOMBA kama kuna aliye athirika na hawa, hata kama bado wanawasiliana hawajafikia hatua ya kufanya biashara husika, itambulike hivyo kuhusu watu hawa, tusaidiane kuwapata kwa wenye weledi huo. NA inawezekana wanapitia UZI huu, Nawaambia Ni kweli kwa Binadamu inaweza kuwa haiwezekani kuwapata kirahisi; Ila kwa Mungu inawezekana, maana hata sasa YEYE anawaona walipo, wanachofanya na hata wana waza nini, Pia Mungu si dhalimu kiasi cha kufanya wengine walie kwa ajili ya utapeli huo na wao wakabaki wanakula BATA tu kwa hela ya maskini (bora ingekuwa ya kifisadi). Muiomba Mungu hujibiwa, haijalishi lini, lakini Mungu anajua na hapendi udhalimu wa aina hii na unaofanana. WARUDISHE PESA ZA WATU. Matapeli jiangalieni, wengine hawatamtegemea Mungu, Ila duniani kuna Miungu HATARI kuliko rehema za Mungu!! watch out!!!

Naomba ushirikiano wenu, na wengine pia msiingie mkenge kwa utapeli wa namna hii: (be warned)

Nimeguswa na maelezo yako na naungana na wewe kutoa namba zinazotumiwa na matapeli katika mtandao wa vodacom katika sekta mbali mbali. mmojawapo ana lafudhi ya kenya na namba zake ni 0758862582.
 
Ulikua una kwepa ushuru sasa yamekutokea puani eti una mwomba Mungu akusaidie!We kweli zwazwa!
 
akienda polisi na yeye atakamatwa, huwezi kwenda kulalamika kwa kutapeliwa katika dili ya kihalifu! Yani polisi wawakamate watu waliokutapeli kwa kutokuuzia gari kinyume na sheria?

Nahisi hujamuelewa kimsingi ni kwamba huwa kuna Magari/Bidhaa ambazo TRA huwa wanaziuza kwa watu walioziagiza kushindwa kulipa Kodi. Kwahiyo its a legal business sio deal wala wizi, bei ya hizo bidhaa huwa inalenga kulipa Kodi aliyoshindwa kulipa huyo aliekuwa Mteja wao
 
duh! Shunghuli ipo
 
hizo bidhaa/magari etc, huwa vinapigwa mnada. Huo ndio utaratibu rasmi. Hayo mengine ni mojawapo ya vieskro vidogo vidogo nchini kwetu.
 
Hii issue TRA na wadau wake wanaijua.
Wapiga dili huwa wanahamishwa na kurejeshwa miaka kadhaa.
Kama mdau mmoja alivyosema ni kwamba pale kuna Camera,watawanasa.
Tatizo ni kwamba kama mnunuzi alienda kununua kwa ahadi ya kukwepa baadhi ya kodi basi hapo kazi anayo.
Na mbaya zaidi,hawa watu wakipiga issue basi kuna wenzao pale bandarini kama maofisa ambao huwapa taarifa ya kila kinachoendelea kuhusu muibiwaji.
Kama ana uhakika mwambie aandike Barua kwa Mwakyembe,maana aliwahi kuwapurua pale kama kuku,sasa na kama mhusika anauhakika juu ya hili basi aandae baru yenye maelezo ya kina na jinsi hao watu wanavyoruhusiwa na TRA kuwa kama madalali pale Bandarini wakati wengine wao sio waaminifu.
Yaani hadi mdada yumo ndani ya utapeli,kweli kazi ipo.Ila Camera zitawaona.
Ila kama ulitaka kukwepa kodi kwa issue,basi hao jamaa usishangae kesho ukawakuta bandarini na wakakugeuka.
Halafu najiuliza kwanza inakuwaje unalipa pesa yote ya gari nje ya ofisi
 
Back
Top Bottom