jingalao
JF-Expert Member
- Oct 12, 2011
- 36,197
- 29,717
Iwapo bunge letu litajikita kwenye kujadili hoja basi tunayo hoja ya msingi sana ya kuijadili.Hoja hiyo inahusu bima ya afya kwa watanzania wote yaani universal health insuarance coverage.
Tanzania lazima ijikomboe na kujitegemea katika sekta ya afya. mfumo bora wa afya unategemea matofali ya msingi yapatayo sita ...hii ni kwa mujibu wa Shirika la Afya Duniani.
Ukiangazia misingi hii unaweza kutambua kuwa Serikali imeendelea kuifanyia kazi kwa kasi na pengine imefanikiwa kwa kiwango kikubwa ingawa bado haijagusa vilivyo msingi wa healthcare financing.
bado tunashuhudia utegemezi mkubwa wa kibajeti ya afya (japo umeendelea kupungua)
Namna ambayo ni bora na pengine hatujaijaribu ipasavyo ni uwekezaji katika sekta ya afya kwa kupitia bima ya afya.
bado chini ya asilimia 40 ya watanzania hawana bima ya afya yoyote kiasi kwamba wakipata shida ya kiafya inawapasa kuharibu bajeti zao na kuingia mfukoni.
bado kuna kundi kubwa la watanzania wanapata huduma ya matubabu kupitia hisani ya wamarekani,waingereza,waswidish n.k
ingawa ukichambua zaidi utakuta wanaomiliki magari na bodaboda wana bima za vyombo hivyo.Hapa unashangaa kuona ukipata ajali utalipwa pikipiki yako lakini hutapata huduma ya kurejesha mfupa kupitia bima.
Katika siku za awali za Mheshimiwa Rais Samia aliwaagiza wataalamu wetu kuchakata kwa haraka na kupeleka bungeni suala la bima ya afya kwa wote ili wanasiasa,serikali na wananchi waamue iwapo ni jambo sahihi au la.
Cha kusikitisha ni kuwa Serikali kupitia mawaziri na wanasiasa kupitia bunge hawakulichukulia kwa hamasa inayotakiwa na badala yake mijadala ya mitandaoni ikatawala.(Yaani wakademka na masuala yasiyo na tija)
Bungeni ukatawala mjadala wa ukosefu wa dawa bila kuangazia poor system ya healthcare financing.
badala yake bungeni pakaibuka mjadala wa kutaka traffic police watolewe barabarani waende kukamata watumishi wa afya(huu ni ujuha kalulu)
Hatuwezi kuwa na dawa muda wote iwapo dawa zikinunuliwa zitaishia kwa wateja wasiolipia by 60 %.hatuwezi kuwa na bajeti ya dawa ambayo italiwa na watumiaji bila kurejea japo sio kwa faida kubwa.
Tunahitaji sustainable healthcare financing.
Sustainable Healthcare financing inakuja kwa njia hizi muhimu.
1-Uchangiaji ghafi wa huduma(user fee)
2-Uwekezaji kupitia bima ya afya
3-Mfuko maalumu kutoka hazina wenye kusudi la kuinua sekta endelevu ya afya.
4-Misaada ya uhisani yenye lengo maalumu na lenye kugusa maeneo korofi lakini yenye uwezo wa kujiendeleza.
Hapa ni lazima tudefine hitaji la misaada ...mfano msaada wa muda maalumu wa ujenzi wa vituo vya huduma,msaada maalumu wa mafunzo ya watoa huduma katika mahitaji yaliyopo na ya msingi n.k
Tuachane na misaada ya condoms na pedi.
Tuachane na misaada ya miongozo ya tiba mpya ili tuuziwe dawa au vifaa.
5-Wananchi kuelezwa wazi kuwa jukumu la afya ni participatory.yaani wasifikiri afya yao ni jukumu la Serikali au wahisani kwa asilimia 100.
Hayati Dr John Pombe Magufuli alitufumbulia fumbo kwa kuanza kujenga miundombinu ya huduma za afya kila kona ya nchi hii...na ameacha legacy kubwa ambayo haitaacha kukumbukwa.
Kazi iliyo mbele yetu sasa ni kuiimarisha Sekta hii ya afya kwa muktadha ninaojaribu kuupigia debe.
Mwaka 2015 kupitia JF niliuliza swali kwa wagombea urais kuhusu ahadi na msimamo wao kwenye swala la bima ya afya kwa wote.
ni bahati mbaya hakuna mgombea aliyeweza kulijibu ipasavyo.
kama mwana mtandao wa kijamii naendelea kuipiga ngoma hii ili wabunge na mawaziri wetu waweze "kudemka " vizuri.
Naamini hata mhe.Rais Samia angependa kuona mdemko wa namna hii bungeni na kwenye jamii.
Jukumu la wapiga ngoma a.k.a wademshaji ni kupiga ngoma sahihi pia.
Nawasilisha.
KWA HISANI YA MTU WA TANZANIA!!