Miongoni mwa mada za kijinga zaidi humu JF huwa ni hizi ligi za kushindanisha Kenya vs Tanzania. Kwa leo haya ndio maoni yangu.
1. Ni kweli Mombasa ni level ya juu zaidi kimandhali kuliko Mwanza. Hilo sina ubishi nalo. Lakini Mombasa ni level ya chini kuliko Dar. Na Dar ni level ya chini kuliko Nairobi. Kama ningeweka mfuatano basi ingekuwa Nairobi-Dar-Mombasa-Mwanza.
2. Miji yote hiyo ya Kenya na Tanzania imejaa uchafu, uholela na zaidi ya 80 ya wakazi wake wanaishi mazingira duni, yasiyopangwa na ovyo kabisa. Hivyo sioni wa kumcheka mwenzake au kujivunia.
3. Maisha yoyote mazuri na kuvutia kwa Kenya yana gharama kubwa na yapo kwa watu wachache zaidi kuliko ilivyo Tanzania. Ni rahisi sana kuishi maisha mazuri ukiwa Tanzania kuliko Kenya. Kuanzia Elimu, Afya, Makazi na Chakula.
4. Wakenya ni watu wenye mtizamo mpana zaidi wa kufanikiwa kimaisha (wapambanaji) lakini mfumo wa maisha yao kijamii hauna furaha wala ladha ya kuvutia ikiwa utawalinganisha na watanzania(waungwana)
5. Kitu pekee kinachoweza kumtofautisha Mkenya na Mtanzania katika mazingira yao ni tabia zao za kijamii lakini maisha yao kiuchumi ni yale yale. Wanafanana, Umaskini mtupu.