Ghazwat
JF-Expert Member
- Oct 4, 2015
- 23,718
- 66,267
Watu kadha wenye silaha walifyatulia magari yaliyokuwa yakisafirisha wanafunzi wa Chuo kikuu cha Kiufundi cha Mombasa (TUM) kutoka kwenye vyumba vyao vya malazi hadi kwenye bewa la Chuo Ukunda.
Afisa wa polisi aliyezungumza shirika la habari la Reuters, lakini hakutaka jina lake litajwe, amesema dereva na polisi wawili wamejeruhiwa.
Afisa huyo amenukuliwa na Reuters akisema; "Basi lilikuwa likiwasafirisha wanafunzi wa chuo kutoka vyumba vyao vya malazi hadi kwenye bewa la Chuo Ukunda kwa masomo na lilikuwa likisindikizwa na gari ndogo lililokuwa na wafanyakazi wa chuo na polisi wawili wa kuwalinda".
Haijafahamika nani alihusika katika shambulio hilo,
Wanamgambo wa kundi la Kiislaam la al-shabab kutoka Somalia mara kwa mara hutekeleza mashambulio Pwani ya Kenya na maeneo ya Kenya yanayopakana na taifa hilo.
Mwaka 2015 walishambulia chuo kikuu cha Garissa na kuua wanafunzi 148.
Majeshi ya Kenya yamekuwa yakikabiliana na wapiganaji hao nchini Somalia chini ya kikosi cha umoja wa Afrika (Amisom)
Nchini Kenya, jeshi la nchi hiyo limekuwa likitekeleza mashambulio katika msitu wa Boni unaopakana na Somalia kuwafurusha wapiganaji ambao wanadaiwa kupanga na kutekeleza mashambulio kutoka katika msitu huo.
Msemaji wa Jeshi David Obonyo alisema wanajeshi hao walipata bunduki sita aina ya AK 47 na risasi 321 wakati wa operesheni hiyo ya kijeshi Bodhei, Boni.
Chanzo: BBC