Mombasa: Mwili wa mtu ambaye gari lake liliingia baharini waopolewa

Mombasa: Mwili wa mtu ambaye gari lake liliingia baharini waopolewa

Suley2019

JF-Expert Member
Joined
Oct 7, 2019
Posts
2,203
Reaction score
5,610
MWILI wa mtu ambaye gari lake liliingia baharini katika kivuko cha Likoni maarufu kama ‘Likoni Ferry’ jana saa nne na dakika 20 mjini Mombasa umeopolewa.

Polisi limemtaja mtu huyo kuwa ni John Mutinda mwenye umri wa miaka 46 na wakati mwili wake ukiopolewa kutoka baharini, mkewe Ruth Mueni alikuwa eneo la tukio.

Shirika la hudumu za Ferry nchini Kenya (KFS), limesema gari la John Mutinda lilishuka katika mteremko kwa kasi ya juu.

Kisa hicho kimerejesha upya kumbukumbu za mkasa mwingine wa mwezi Septemba mwaka huu ambapo Mariam Kighenda na mwanawe Amanda Mutheu walikufa maji.

Iliwachuku waokoaji takriban siku 13 kuopoa miili ya Mariamu na mwanae pamoja na gari walilozama nalo.

Taarifa ya KFS kuhusu kifo cha Mutinda ilisema: Dereva alikuwa akiendesha gari aina ya saloon ambayo namba zake za usajili hazijawekwa hadharani.

Kwamba baada ya kununua tiketi aliteremka kwa kasi katika mteremko wa feri na kuingia baharini.

Shirika hilo liliongezea kwamba dereva huyo alikataa kusimamisha gari hilo licha ya juhudi kadhaa za maafisa wa feri kumsimamisha.

Maboti ya uokoaji ya KFS, wanamaji wa Kenya ‘Kenya Navy’ na maofisa wa polisi wakishirikiana na waokoaji wengine yalifika katika kivuko hicho mara moja na kuanzisha operesheni ya kulisaka gari hilo.

Gavana wa Mombasa, Hassan Joho mapema alikuwa amesema kwamba Serikali ya kaunti hiyo ilikuwa imepeleka kitengo chake kushirikiana na waokoaji wengine wa idara tofauti za Serikali.

Chanzo: Mtanzania


 
Back
Top Bottom