Suley2019
JF-Expert Member
- Oct 7, 2019
- 2,203
- 5,610
Inadawa Real Madrid imekubaliana na AS Monaco kumnunua Aurelien Tchouameni (22) kwenye usajili utakaogharimu jumla ya zaidi ya Paundi Milioni 85 (Tsh. 249,405,355,250).
Klabu za Liverpool, Manchester United na PSG zilikuwa zinamuwania pia mchezaji huyo aliyejiimarishia nafasi katika kikosi cha timu ya taifa ya Ufaransa kwa miezi tisa iliyopita.
Kiungo huyo alianza maisha ya soka katika Klabu ya Bordeaux, na kisha kujiunga na AS Monaco Januari 2020 na kuweza kushinda tuzo ya Mchezaji Bora Mdogo katika Ligi Kuu ya Ufaransa.
Kwa usajili huu, timu gani itaweza kufikia ubora wa Kiungo cha R. Madrid?