Monday Morning Special!!

Mzigua90

JF-Expert Member
Joined
Sep 23, 2014
Posts
38,342
Reaction score
88,625
Nilivyojiunga JF nilijua ni sehemu nitasoma niburudike na nijifunze. Sikua najua hata members huwa wanaonana nje ya hapa. Kumbe watu huwa wanaonana huko nje halafu yakiwabumia wanarudi kutuelezea humu.

Inatosha kuwa mtu mzima kujua kipi niweke wazi kwenye mtandao kipi nisikiweke wazi. Kwa mimi naona ni jambo baya kuweka ugomvi wa matusi na mahusiano kwenye mtandao ambao hujui nani utakutana nae kesho.

Ukiwa kwenye ugomvi unaoweza kuuepuka uepuke. Heri nusu shari kuliko shari kamili. Hutaonekana mnyonge kwa kumdharau mtu anaekukosea. Hata huyo mtu akiandika mara mbili tatu akiona humjibu ataacha tu.

Umetengeneza marafiki kaa nao kwa amani. Kupishana ni jambo la kawaida kwa binadamu. Usitake kupishana kwako kidogo na mtu kuwe ndo bifu ulibebe mgongoni.

Tuifanye JF kuwa sehemu salama. Tukumbuke kuna maisha baada ya mitandao. Maisha hayaishii leo hapa JF. Kuna kazi kuna watoto kuna ndugu. Usijiangalie wewe unaendika ujinga humu. Angalia na wengine walio nyuma yako.

Hakuna mtu aliepewa medal kwa kupenda kutukanana mtandaoni sana sana watu wanakudharau.

Nashangaa JF niliyoingia kwa mapenzi yangu watu wanachaguliana wa kuongea nae wa kucheka nae. Guys huku uliingia mwenyewe. Usifanye jambo kumfurahisha mtu ulomkuta humu ambae hakuchangii hata bundle. Mtu anakwambia kamtukane mzigua na wewe kwa kuwa akili yako haijui kuchanganua mambo unakuja unanitukana kweli.

Huku ni home of GT embu tuishi basi kama GT.

Nimesema haya baada ya kuona watu wanajisahau sana na hii mitandao hasa humu.
 
Word. Maisha kujiachia bana. Sio unafiki mtu anachochea ugomvi akiona heee yanakaribia kumrudia ndo anakurupuka Kuita mods futeni wakati huo alikua anainjoi mwanzo mwishoView attachment 782401
Hao wanaochochea trust me wanakuaga hata hawaelewi kinachoendelea. Wabaya ni wale wanaojua kinachoendelea halafu wanatumia wengine waendeleze ugomvi.
 
Mzigua90 hili jukwaa halina tofauti na maisha ya mtaani rafiki. Kuna watu wa hulka zote....wanaojielewa, wahuni, wajuaji wastaarabu, washari..yaani sampuli zote. Umeandika vizuri lakini unaweza ukaogelea matusi vilevile. Lakini umefanya jukumu lako.

Cha msingi ni kuwa makini na kuwa na utu na ubinadamu kwenye kila tulifanyalo, ile sheria naipenda sana, watendee wengine kama ambavyo ungependa wao wakutendee wewe.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…