Nimecheka jinsi mnavyolazimisha wanafunzi kuvaa minguo yenu na kuwaamrisha waende kujaza uwanja eti mseme wafuasi wengi wamehudhuria.
Enzi mimi nasoma mbona CCM hamkuwa na ujinga huu? Niliwahi kuhudhuria mikutano yenu hasa kampeni za Ubunge bila kushurutishwa na nikiwa na Uniform za Shule kama kawaida bila kuvalishwa Minguo yenu hiyo...
Hivi hizi ndio kampeni za kisayansi kweli za kulazimisha na kusomba watu...
Wenye akili zao wanachora tu huku wakiendelea kuwalia hela zenu(ambazo ni kodi za watanzania wote).
Kinachowabeba ni ushindi kwa msaada wa polisi,TISS na TUME tu.