“MONEY LAUNDERING” inaweza kukuza uchumi wa nchi au Jiji?

“MONEY LAUNDERING” inaweza kukuza uchumi wa nchi au Jiji?

Unaambiwa London ndo capital ya money laundering dunia.Nadhani kuna namna mji unafahamika sidhan kama wameshindwa kuzia

Sehemu kama dubai yaan easy mazingira rahisishi yapo
I get you ila huko circular flow ya hizo cash lazima iwe complex juu kuna mamlaka zinafatilia sio kama huku simple tu hela inatakatishwa na hamna mtu anakuja kuuliza
 
Nauliza hili nikiwa na sababu.

vita ya Ukraine imeibua mengi sana!!Yote tisa kulikua na hili la utakatishaji pesa ambao mji wa London kwa makusudi ulikua umetoa muanya kwa matajiri wengi hasa vigogo wa Russia.
Kwa sasa London inasemekana ni

“Money Laundering Capital of the world”

London unaweza kutengeneza shell compan au kampuni bubu na kununua mijengo au kuwekeza kwenye Real Estate bila kujulikana nani mmiliki kupitia hyo kampuni bubu ambayo kiuhalisia haipo.

Kiufupi ni mahali pekee unapoweza kuingiza mabilioni na kuyawekeza bila kuwa na trace ya mmiliki, umetoa wap n taarifa nyingine kama hizo .Na kuna mifumo wezeshi ya hivo kukusaidia kuficha utambulisho wako.

Wakati dunia nzima utakatishaji wa fedha ukiwa n haramu na wenye madhara kwa uchimi ila London imeuruhusu na kuutengenezea mazingira ya kuustawisha.Ni vita ya ukraine pekee ndio kwa lengo la kuwadhoofisha marafiki wa Putin ndipo walianza kuwafuatilia.

Sehemu nyingine ambako watakatishaji wa fedha hukimbilia ni Dubai.Pia kuna mazingira wezeshi ya kutakatisha fedha.

Kwa wataalam wa fedha!

Je Kuna faida zilizofichika za kutakatisha fedha kwa nchi au mji???
Kama hamna kwanini miji mikubwa kama hii itengeneze mazingira wezeshi na ilihali inaweza kuzuia.?View attachment 2870759
Money Laundering ni uhalifu yaani, criminal offence.

Huwezi kutoa fedha kwenye rushwa, ufisadi, biashara ya madawa na njiazingine za kihalifu kisha ukaziweka kwenye mzunguko rasmi wa fedha hiyo ni money laundering.

Hata hivyo kwa sasa financial regulations za Ulaya zimebadilika sana na hakuna kutia fedha kwenye FS bila kutaka kujua chanzo cha fedha hizo.
 
Back
Top Bottom