Umakini wa post yako kiongozi siuoni lakini kwa kusaidiana kuongea kama kijiweni nitakujibu kwa swali, je ni lazima upeleke pesa benki?kwa mfano niki okota milioni mia (ignore the odds), nikaamua kupeleka benki wanaweza kuzi fungia kwa kudhania ni fedha haramu.
NB:
assume nilikua na savings account ambayo haikuwahi kuwa na zaidi ya milioni tatu kwa wakati mmoja.
Na source ya hizi milioni mia ni "kuokota"
Itakuwaje wana jf
Wakati unafungua akaunti kuna fomu ulijaza,zina maelezo hata chanzo cha kipato chako,kwa hio ni lazima wajiulize kulikoni?
Ina maana watanihifadhia hizo hela bila tatizo lolote.
Ukiwaeleza vizuri jinsi ulivoziokota hawatakubana na watakuhifadhia na hata ukitaka ushauri wa kuweka Akiba kwenye Akaunti maalum watafurahi sana.
Hawa Wachimbaji wa Madini na vito wanapata hata zaidi ya hizo, na Benk sio kazi yao kuchunguza umezipataje
Ngoma ni hapo utakapofungua akaunti ya Biashara (Current account) ni lazima uwe na TIN ndipo TRA wanauhalali wa kujua umezipataje na POLISI wajue nani kapoteza
Money Laundering ni UTAKATISHAJI (ufuaji nguo km kwa Dobi) na zipo aina nyingi mpaka hizi za Wizi wa Electronic (ambapo BOT wanataka kusimamisha)
Kwa uelewa wangu huo utakatishaji ni A/c yako inajazwa Hela kutoka mahali km wamekosea ukaokota (Mfano a/c za Serikali, Mashirika ya Umma nk0 na baada ya siku chache wakaziondoa wewe uliyezipitisha katika A/c yako utatafutwa na kuisaidia POLISI, Benki, BOT na hata TRA
Mi nadhani siyo lazima upeleke zote kwa mkupuo! Peleka kidogo dogo, but lazima ubuni kijimradi ya kuzugia, ili hata kama wakikushtukia, basi ujue jinsi ya kujhdefend.
Mh...! Tehe tehe tehe, najishangaa navyotoa maelezo kana kwamba tunachojadil ni real Money