GE2025 Money VS Power: Siri ya Matajiri na Watu maarufu kuutaka Ubunge Tanzania

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025

MR BINGO

JF-Expert Member
Joined
Feb 12, 2016
Posts
1,215
Reaction score
2,614
HELLO JF

Wiki hii kumekuwa na wimbi kubwa la watu maarufu na matajiri kukimbilia kuchukua fomu za kugombea ubunge, jambo lililoibua mijadala mitandaoni huku wengi wakiuliza: "Kuna siri gani kwenye Ubunge?"

Inawezekana sababu mojawapo ni uchu wa kuwatumikia wananchi, lakini ukweli ni kwamba watu maarufu na matajiri wachache sana hujitokeza kweli kwa ajili ya kutatua kero za wananchiβ€”asilimia 1 hadi 2 tu.

Sababu ya pili inayotajwa ni kutafuta kipato. Ingawa ubunge una maslahi, kwa mazingira ya Tanzania ni lazima kutumia pesa nyingi ili kuupata. Hivyo, mtu anayetafuta pesa hawezi kuupata kirahisi, hasa ikizingatiwa kuwa wengi wanaotaka ubunge tayari wanaingiza fedha nyingi zaidi ya mshahara wa mbunge.

Sababu kubwa zaidi ya watu kukimbilia ubunge ni madaraka (power). Ubunge unafungua milango ambayo hata pesa haiwezi kufungua. Madaraka huleta connectionβ€”mfano mzigo wako ukikwama barabarani au bandarini, badala ya kuhangaika, unavuta waya kwa waziri au naibu waziri na mambo yanaenda. Huu ushawishi wa madaraka ndio unawavuta wengi kuliko kipato au nia ya kusaidia wananchi.

Your browser is not able to display this video.
 


Yaani unaweza kumfananisha Mfanyabiashara ambaye ana run biashara za Mbalion na Mbunge mwanasiasa .


hao unaowaona kina Abud ,msukuma n.k wote hao wanafata hela bungeni and nothing else
 
Yaani unaweza kumfananisha Mfanyabiashara ambaye ana run biashara za Mbalion na Mbunge mwanasiasa .


hao unaowaona kina Abud ,msukuma n.k wote hao wanafata hela bungeni and nothing else
Bungeni kiinua mgongo cha miaka mitano puls mshahara na posho ya kila mwezi ni 700ml. Aboud anashusha kila baada ya miaka mitatu mabasi 100 kwa mkupuo na kila bus ni 300ml. Piga hesabu zako halafu uone kama ubunge unaweza kukupa pesa hata ya mabasi matatu mapya. Mtoa mada yupo sahihi.
 
Yaani unaweza kumfananisha Mfanyabiashara ambaye ana run biashara za Mbalion na Mbunge mwanasiasa .


hao unaowaona kina Abud ,msukuma n.k wote hao wanafata hela bungeni and nothing else
kwa hiyo wewe unaamni kuwa Shabiby anaenda kutafuta milioni 12 na posho ya laki tatu kwa kikao bungeni na kiinua mgongo cha million 250 baada ya miaka mitano?wakati anaweza kuwa na mfanyakazi anayeingiza hicho kipato kwa mwezi
 
Unchobidi kujua hao wanafata hela na kingine wanaingia bungeni Ku-secured biashara zao.

Ikiwa hawafati hela waambie watumie mishahara yao na kiinua Mgongo kuisadia jamii kama watakubali.
 
Yaani unaweza kumfananisha Mfanyabiashara ambaye ana run biashara za Mbalion na Mbunge mwanasiasa .


hao unaowaona kina Abud ,msukuma n.k wote hao wanafata hela bungeni and nothing else
Mbona Rostam na Mo pia walikuwa wabunge pamoja na utajiri wao?
 
Unchobidi kujua hao wanafata hela na kingine wanaingia bungeni Ku-secured biashara zao.

Ikiwa hawafati hela waambie watumie mishahara yao na kiinua Mgongo kuisadia jamii kama watakubali.
Nakuunga mkono point ya ku-secure biashara zao. Kusaidia jamii ni kama huku mtaani tu tunavowatreat ombaomba wapo wanaotoa na wapo wanaowabeza inategemea moyo wa mtu.
 
kwa hiyo wewe unaamni kuwa Shabiby anaenda kutafuta milioni 12 na posho ya laki tatu kwa kikao bungeni na kiinua mgongo cha million 250 baada ya miaka mitano?wakati anaweza kuwa na mfanyakazi anayeingiza hicho kipato kwa mwezi
Haendi kutafuta Ila mwambie huo mshahara awe anaurudisha kwa jamii .

Nenda katika Mjimbo yao hata visima vya Maji vinawashinda kujenga .

Watu wanafata hela na hela ya ubunge ni moja ya biashara yake inayomuingizia mapato.

Ingekuwa hawafati hela tusingewaona wanapambania kurudi kila muhula.
 
Mbona Rostam na Mo pia walikuwa wabunge pamoja na utajiri wao?
Kwahiyo ukiwa tajiri hautaki hela ?

Hao wote wanafafta hela na pia wana-secure biashara zao hasa katika mambo ya kodi.
 
pesa ni mojawapo ya sababu lakini siyo sababu kuu ya wao kuhangaika na huo ubunge maana ukifanya comparison ya Kipato chao na pesa inayopatikana bungeni bado ni mbingu na ardhi
 
Mil 12 ambayo unaipata kwa kugonga meza kila mwezi ni hela nyingi Sana .

Kwa MTU anayefanya biashara anaelewa
 
Maybe ume-overlook kitu kimoja, utofauti wa hela na utajiri.

Kuwa na hela nyingi haimaanishi wewe ni tajiri, na kuwa tajiri ni mpaka uwe na power juu ya eneo au segment/kundi fln la watu.

Najua hujanielewa ngoja ninene kwa mifano. Ukiwa na frames au nyumba kkoo, ofcoz unaweza pata hela saaana tu kupitia kodi za wapangaji, mabilioni, lakini huo haujafikia level ya kuitwa utajiri (japo watu wengine wanadhan ni utajiri). Lakini chukulia mtu kama MO au Bakhresa, wao wanalisha Tanzania nzima, thats power, thats utajiri sababu wana control kubwa sana kwenye food supply. GSM nae anaingia huko sio sabab ya Profit, ni sabab anataka share yake kwenye hio control/power

Kwa Geopolitics fikiria wanaocontrol supply ya mafuta, thats power which creates wealth.

In Summary,
Hela nyingi sio utajiri, utajiri halisi unaanzia ukiweza ku-secure power au control juu ya kitu fln, so ni power first then wealth, sio wealth then power kama andiko lako linavyoashiria.

Hao unaoona wanakimbilia ubunge ukifuatilia zaidi kiundani utagundua sio matajiri lakini wana hela nyingi.

Ukiwa tajiri wa kweli hata wanasiasa na watawala watakuabudu, nadhan uliona Elon na Trump. Au fuatilia Dangote na serikali ya Nigeria.

So forget about 'Money is Power', Power is Power and Power creates Wealth
 
pesa ni mojawapo ya sababu lakini siyo sababu kuu ya wao kuhangaika na huo ubunge maana ukifanya comparison ya Kipato chao na pesa inayopatikana bungeni bado ni mbingu na ardhi
Sawa Ila waambie tu wachukue Pesa wanayolipwa Bungeni wairudishe kwa jamii uone Kama watakubali.

Hao jamaa ni opportunity seeker na money hunter .
 
100%

Nadhani mtoa mada hapa atajifunza kitu.
 
kwa hiyo wewe unaamni kuwa Shabiby anaenda kutafuta milioni 12 na posho ya laki tatu kwa kikao bungeni na kiinua mgongo cha million 250 baada ya miaka mitano?wakati anaweza kuwa na mfanyakazi anayeingiza hicho kipato kwa mwezi
πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚ Hio pesa labda ni ya ku transfer kwa wajukuu kwenye akaunti zao
 
kwa definition yako ya utajiri uliyoitoa hapa it means Tanzania hakunaTajiri hata mmoja maana sijaona Tajiri anayeweza kutunishiana misuli na mwanasiasa wa caliber yake ya utajiri including Huyo MO na bakhressa
 
Kwahiyo ukiwa tajiri hautaki hela ?

Hao wote wanafafta hela na pia wana-secure biashara zao hasa katika mambo ya kodi.
Ndio unarudi sasa kwenye point namba 3 ya mtoa mada (power). Wanapata kitu ambacho pesa pekee haiwezi kuwapa.
 
Yaani unaweza kumfananisha Mfanyabiashara ambaye ana run biashara za Mbalion na Mbunge mwanasiasa .


hao unaowaona kina Abud ,msukuma n.k wote hao wanafata hela bungeni and nothing else
Sasa we ndiyo umeandika nini. Abood au Shabiby anafuata 18M kwa mwezi? Think big, jibu liko kwenye Maslow's hierarchy of human needs
 
Hiyo 700M we umeitoa wapi, shida ya huku kila mtu mjuaji
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…