PreGE2025 Mongella awataka Wanachama wa CCM kudumisha amani kuelekea Uchaguzi Mkuu Oktoba 2025

PreGE2025 Mongella awataka Wanachama wa CCM kudumisha amani kuelekea Uchaguzi Mkuu Oktoba 2025

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla)

Waufukweni

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2024
Posts
5,383
Reaction score
18,776
Naibu Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Bara, Ndugu John Mongella, amewataka wanachama wa chama hicho kudumisha amani na utulivu kuelekea Uchaguzi Mkuu wa mwaka huu.

Akizungumza, Machi 24, 2025, jijini Arusha kwa niaba ya Katibu Mkuu wa CCM, Balozi Dkt. Emmanuel Nchimbi, Mongella amewahimiza wana-CCM kuwa makini na kuepuka vishawishi vinavyoweza kusababisha vurugu. Amesisitiza kuwa huu ni wakati wa kuwa imara, akibainisha kuwa Tanzania ina heshima ya kipekee barani Afrika kutokana na utamaduni wake wa kudumisha amani na utulivu.

Kupata taarifa na matukio yanayojiri kuelekea uchaguzi mkuu kwa kila mkoa ingia hapa: Special Thread: Mijadala na Matukio ya Uchaguzi Mikoa yote Tanzania Bara na Zanzibar kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025

Katika hotuba yake, Mongella ameipongeza Jumuiya ya Wazazi kwa kuandaa kongamano hilo la kumpongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, kwa kutimiza miaka minne ya mafanikio katika uongozi wake.

Aidha, ameisifu jumuiya hiyo kwa mikakati yake madhubuti ya kukihami chama na kuhakikisha CCM inapata ushindi katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka huu.

 
NO reform No election.

Kichwa cha habari toa neno AMANI weka UCHAWA itaketa maana zaidi.
 
Back
Top Bottom