LeopoldByongje
JF-Expert Member
- Apr 28, 2008
- 372
- 13
ili inabidi aulizwe popote atakapo-onekana akikatiza ili isiwe ni sawa na kujaza gunia maji. Linahusika sana coz hizi gharama ni kubwa sana!!
Ni kweli gharama ni kubwa mno na kwa hesabu ya haraka zimeishafikia zaidi ya Bilioni moja na ushehe. Hatujui mpaka kesi inamalizika zitafikia kiasi gani. Thamani ya samaki hao ni kama Bilioni Mbili. Kwa hili Mheshimiwa Magufuli asilaumiwe. Watendaji wake ambao naona ni Mawakala wa Wenye viwanda vya kusindika minofu ya samaki walimzunguka na kumuingiza mkenge. Kwa hali ya kawaida Samaki hao ilitakiwa wahifadhiwe Chuo Cha Uvuvi Mbegani - Bagamoyo ambapo kuna Majogofu (Cold rooms) yenye uwezo wa kuhifadhi samaki hao; hata japo kwa malipo badala yake wakaamua samaki hao wakahifadhiwa kwenye Majogofu ya Mfanya biashara binafsi aitwaye Bhagat? Hii ni hujuma!!!.
Mahakama zetu nao wamechangia naona kwa kukosa uzalendo. Kwa kuwa Mahakama zina uwezo wa kuruhusu samaki au mali ambayo inaweza kuharibika (perishable) iuzwe na fedha zikatiwe sitakabadhi ya Serikali ambayo inatumika Mahakamani kama Exhibit. Kwa nini Hakimu aamue kusitisha zoezi la mnada kwa kisingizio kuwa Mahakama yake ni mamlaka ya chini na kwamba anataka samaki hao waoneshwe kama ushahidi kwenye Mahakama za juu!! Kwani hilo hakulijua tangu siku ya kwanza alipopokea kesi hiyo?? je kusingekuweko huduma ya kuwahifadhi hao samaki angechukua uamuzi gani?
Wadau kuna maswali mengi kuliko majibu. Lakini yote hayo ni dalili za ufisadi na Hujuma kwa Taifa letu.