Monitoring thread: John Pombe Magufuli katika Awamu ya Nne

ili inabidi aulizwe popote atakapo-onekana akikatiza ili isiwe ni sawa na kujaza gunia maji. Linahusika sana coz hizi gharama ni kubwa sana!!

Ni kweli gharama ni kubwa mno na kwa hesabu ya haraka zimeishafikia zaidi ya Bilioni moja na ushehe. Hatujui mpaka kesi inamalizika zitafikia kiasi gani. Thamani ya samaki hao ni kama Bilioni Mbili. Kwa hili Mheshimiwa Magufuli asilaumiwe. Watendaji wake ambao naona ni Mawakala wa Wenye viwanda vya kusindika minofu ya samaki walimzunguka na kumuingiza mkenge. Kwa hali ya kawaida Samaki hao ilitakiwa wahifadhiwe Chuo Cha Uvuvi Mbegani - Bagamoyo ambapo kuna Majogofu (Cold rooms) yenye uwezo wa kuhifadhi samaki hao; hata japo kwa malipo badala yake wakaamua samaki hao wakahifadhiwa kwenye Majogofu ya Mfanya biashara binafsi aitwaye Bhagat? Hii ni hujuma!!!.

Mahakama zetu nao wamechangia naona kwa kukosa uzalendo. Kwa kuwa Mahakama zina uwezo wa kuruhusu samaki au mali ambayo inaweza kuharibika (perishable) iuzwe na fedha zikatiwe sitakabadhi ya Serikali ambayo inatumika Mahakamani kama Exhibit. Kwa nini Hakimu aamue kusitisha zoezi la mnada kwa kisingizio kuwa Mahakama yake ni mamlaka ya chini na kwamba anataka samaki hao waoneshwe kama ushahidi kwenye Mahakama za juu!! Kwani hilo hakulijua tangu siku ya kwanza alipopokea kesi hiyo?? je kusingekuweko huduma ya kuwahifadhi hao samaki angechukua uamuzi gani?

Wadau kuna maswali mengi kuliko majibu. Lakini yote hayo ni dalili za ufisadi na Hujuma kwa Taifa letu.
 


john pombe magufuli for presidency 2010...
 
john pombe magufuli for presidency 2010...
Huyu bwana bado ni tishio kisiasa!

Mwaka juzi walimpiga vita sana hapa JF, akazushiwa vijikashfa vingi sana, hata wakati fulani wakasema amefariki. Nafuu aliyonayo sasa hivi ni kwamba sisiemu-MTANDAO wamelala mbele kuogopa vita dhidi ya ufisadi.

Unawaita warudi?
 

WanaMtandao walikuwa, na bado wanatafuta jinsi ya kumuondoa J.P.Magufuli (JPM) kwenye Cabinet. Kwanza wanataka kuanza kwa kum-discredit mbele ya public ili hatimaye wakimuondoa pasiwe na kelele nyingi.

Inafahamika fika kuwa uamuzi wa kuuza nyumba za Serikali ulikuwa wa Serikali kuu ya B.W.Mkapa, na ulipitishwa na Cabinet, Kikwete naye akiwemo ndani ya Cabinet. By the way Kikwete naye amechukua nyumba ya Serikali. Magufuli alitangaza kwa kuwa zilikuwa chini ya Wizara yake.

JPM ni kiongozi mtendaji halisi popote pale, iwe Ujenzi, Ardhi au sasa Samaki/Nyama (sic!), na hii ni threat kwa watu fulani. Period.
 
Nitaridhika akiondolewa Mramba sio magufuli.

Nimuhimu pia uchunguzi ufanyike maana Magufuri katumia vibaya madaraka kwenye miradi ya barabara akiwa waziri wa miundombinu, vilevile akiwa ardhi si safii kabisaaa
 
Waziri magufuli anatakiwa kuwekwa wizara ya mambo ya ndani na Masha anatakiwa kuachishwa kazi. Huyu Kijana anatutia aibu sana na ni kitu cha kushangaa kwamba ni kizazi kipya. Hakuna mtu anamwamini Masha hivyo ningependekeza Masha kutolewa na nafasi yake kuchukuliwa na Magufuli.
 

Kwa nini unaona Magufuli anafaa kwenye wizara hiyo? Lazima useme umetumia vigezo gani au umeangalia nini mpaka kufikia kuona hivyo. Kwa nini awekwe wizara ya mambo ya ndani na si wizara nyingine?
 
Mwanafalsafa;

Si dhani kwamba wewe ni mtoto sana kiasi kwamba wakati magufuri akiwa wizara ya ujenzi hukuwa unajitambua.Kamundu hana haja ya kutaja au kusema kwanini magufuri awekwe nafasi ya masha.Mambo aliyoyafanya akiwa miundo mbinu yanafahamika, sasa unataka ataje nini.Kama enzi za magufuri ulikuwa mtoto mdogo basi ulizia watu wakwambie alifanya nini.

Masha, mimi binafasi sioni anafanya nini na kazi gaini zaidi ya kutapatapa kwenye nafasi aliyopewa.JK,sijui kama kwanini hajaliona hilo,watu wanaingia Tanzania kufanya kazi kumbe wanapita immigration kuwa wanakuja kutembea Tanzania kumbe wanakuja kupiga mzigo Tanzania alafau nyie ndo wa kwanza kulalamika wachina wamejaa kariakoo,sijui wazungu wamejaa tanzania nani anawaopitisha kama siyo yeye na staff wake.
 

I still stand by what I said. Kwa nini kaona atafaa wizara ya mambo ya ndani? Kufanikiwa wizara ya ujenzi haimaanishi ata fanikiwa wizara ya mambo ya ndani.

Na pia swali lingine ni kwamba kwa nini kaona apelekwe wizara ya mambo ya ndani na si wizara nyingine? Kwani ni wizara ya mambo ya ndani tu ndiyo yenye waziri aliye boronga?

Hatuwezi kuassume kuwa mawazo ya mtoa mada itakua sawa na ya kila mchangiaji. Swali langu halina tatizo lolote. Kaja na kasema Magufuli ahamishwe huko sasa kwa nini asiseme why? Na itambulike sijasema Magufuli hata fanikiwa huko ila ina paswa aseme why he feels magufuli should be there. Sasa wewe unakuja na kusema tu hujaona mafanikio yake wizara ya ulinzi?

There is no problem with my question mkuu.
 
Mwanafalsafa;
Wewe binafisi unaona masha anafanya kazi nzuri sio.Mimi nilivyomwelewa huyu bwana ni kamba wizara ya mambo ya ndani ni nyeti sana.Ukiangalia swala zima la utitili wa watu wanaotinga Tanzania mpaka madreva kuja kufanya kazi Tanzania na khali tunao madreva wa kutosha hapa na wenye uzoefu.Na wanapita borders kwa kuja kutembea tu.Ndo huyu bwana akaona nafasi hii afadhali apewe mtu strict,kama magufuli.Toa pendekezo lako na wewe jinsi unavyoona lakini sio kupinga hoja mojakwamoja, inaonekana imekukela kabisa hiyo.
 

Mkuu mbona unaspin mambo? Sijasema Masha anafanya kazi nzuri nimemuuliza kwa nini anaona Magufuli anafaa. Wewe unaona nimefanya kosa kuuliza hilo? Haha wewe ndiyo umekereka mkuu. Yeye kamtaja mtu na hajatoa sababu sasa kuna ubaya kuhoji kwa nini anafaa? Kama nilivyo sema mkuu sijakataa pendekezo lake I simple asked yeye kwa nini anaona anafaa na sidhani mtoa mada anakuhitaji umjibie.
 
Binafsi natambua mfumo wa uongozi tulio nao hauna dira ya kutupeleka pale tunapotaka kimaendeleooo...mkuu wa kaya hawezi kukiri eti 30% ya bajeti kupitia manunuzi inakwenda mifukoni kwa wachache tena wanajulikanaaaa..

kubadili masha ya magufuli bado ni sawa tuu bila kufanya hata utafiti wa vigezo kwani pamoja na mfumo unaochochea uzembe kaziniii..magufuli amejitahidi kuwa action oriented na kusonga mbele kuliko wenzake wotee kwa sasa ndani ya cabinet!!!!!

haitoshi kumbadili na masha kwani anastahili kuwa kiranja mkuu kwa mazingira ya uzembe wa sasa tulio nao..(mapungufu yake bado sio kikwazo cha maendeleo)
 

Wewe sema madhambi ya Masha na PENDEKEZA aachishwe kazi Maghufuri sio muarobaini, wako watu wengi hata Anne Kilango. muacheni Maghufuri wetu asimamie KITOWEO kwanza ndio aondoke aje kuwa RAIS wetu 2020.
 
Kwanini Magufuli kwanini usiwe wewe au yule na yule! kuna zitto, hamad rashi etc....embu tuibue vipaji vingine ati! magufuli is about to retire.
 


Kwa mtazamo wangu naona bado magufuli hastahili wizara ya mambo ya Ndani. Kwake wizara inayomstahili ni kama fedha au wizara yoyote inayoshughulika moja kwa moja na kuongeza pato la taifa na yenye kuhitaji usimamizi makini. Nafikiri madini kunamfaa zaidi kuhakikisha tunapata hela za kutosha na kukuza pato la taifa. Au tumrudishe infrastructure ambako kuna uozo kem kem
 
Shangazi bado hatujamaliza Project yetu Chalinze-Msata-Segera, pls
 

Hapa mkuu sawa, kama mh magufuli au mtu mwingine yoyote wa aina yake angepelekwa kushikilia wizara ya madini, sidhani hata kama issue ya north mara ingekuwa story leo achilia mbali umaskini tuliojitengenezea kwa kwa kubadilishana madini na mahandaki.
 




Mambo anayopenda sana Mh Masha ! kwa haya anafaa sana kuliko nafasi aliyo nayo kitaifa!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…