Wakuu, tujaribu kuupitia utendaji wa Magufuli katika awamu ya nne na kwa kuanzia naanza na makala hii kutoka gazeti la Tanzania Daima
JANA vyombo vya habari nchini vimechapisha taarifa za ajabu. Taarifa hizi zinasema Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, John Pombe Magufuli, ametishiwa kuuawa na waandishi wa habari.
Waandishi anaowatuhumu ni Mhariri Mtendaji wa Habari Corporation, John Bwire, Mhariri wa Rai, Muhingo Rweyemamu na mwandishi wa Rai, Neophitius Kyaruzi. Ametoa taarifa polisi Dodoma Julai, mwaka huu na kupewa RB namba DO/IR/3085/2006.
Katika mashitaka yake, anasema wahariri hao na mwandishi huyo wamemtishia kwa kutumia SMS kuwa watamuua.
Wao katika utetezi wanasema waliwasiliana naye kupata ufafanuzi juu ya taarifa za barabara ya Usagara hadi Geita, zilizoonyesha kuwa kuna mahali hakutenda kwa usahihi, hali iliyoitia serikali hasara.
Source: Tanzania Daima
Alafu watu wanashika pango eti jembe? Waziri mzima andanganya ilikuwazima Waandishi wasiripoti upotefu wa Mapesa yetu. Jeuri hiyo na bado yuko nayo ''Wasio na Pesa wapige mbizi''-Kigamboni Dsm