Monitoring thread: John Pombe Magufuli katika Awamu ya Nne

Monitoring thread: John Pombe Magufuli katika Awamu ya Nne

Kwahiyo Lowassa ni muadilifu..??
Mwadilifu sana,aliwajibika kuiokoa serikali.
Leo mmemtosa mkimhamishia kawama zote yeye huku mkiogopa kumpeleka mahakamani.Sasa ngojeni awaonesheni mabadiliko
 
Nilimsikia huyo makufuli kwenye mkutano wa shinyanga anawaambia watu huyu mgombea wa ubunge Ccm alisoma na mdogo wangu Mussa kwa hiyo nitamuongezea na km 10, siwezi kumwangusha,,nikachoka
 
Kufananisha ufisadi wa magufuli kama upo na ufisadi wa lowasa ni sawa na kulinganisha mlima Kilimanjaro na kichuguu au mto Amazon na mfereji.

Toeni masihara yenu hapa.
 
Kumbe hata hujuwi unaloongea.mali za serikali zinauzwa kwa yeyote atakaefika bei awe mtumishi au mwanafunzi.it doesn't matter who you are.so long as the government collects its share

Mkuu,Lowassa anapoimba Elimu,Elimu.Elimu ina maana kubwa kwako ila wewe hujui tu!
 
Sio tatizo kumuuzia mdogo wake nyumba. Kumaliza chuo tu sio sababu ya kutokuwa na pesa. Mussa Magufuli ni mtanzania kama watanzania wengine. Swali ni je, who was eligible to buy?

Hakua eligible, sheria ilikua inatamka wazi awe ni senior civil servant, sasa mtu hata hajaajiliwa aliuziwaje nyumba?

Vile vile mpenzi wake ambae alikua sio mtumishi aliuziwaje nyumba, hapa ishu sio utanzania, ishu ni utaratibu na matakwa ya sheria ya uuzaji nyumba zilipindishwa na magufuri mwenyeee.
Mtu kama huyo hafai.
 
Bora ungekaa kimya kuliko kuandka pumba afu unaanza na kumaliza na kingereza utafikri mjuaji kweli hivi kna mali ya umma itauzwa bila masharti???
Mbna kila mwenye hela angeenda kununua!!! Kichwa kisichokuwa na akir ni mzigo kwa miguu

Sure mkuu huyo barafuyamoto hana akili, kichwa kinalemea miguu.
 
Last edited by a moderator:
Kamùulize babu yako anayefaa alipata wapi hela za kununua nyumba uingereza tena London? Na kwanini asingenunua humu tanzania kama yeye mzalendo? Bora magufuli anawekeza nchini kwake. Mzobe Mzobe na magufuli hadi magogoni

Vijana va ccm hamuwezi kuwaza, vichwani mmejaza mav.i na kazi ya kuwaza mmemuachia nape na makamba wote walufeli hata moja ongeza moja hawajui,nape alipata sifuri, makamba akaiba mtihani leo ndio think tank ya vijana wa ccm.

Kama jiniasi ndani ya ccm ni nape unategemea nini, mzee mwenye busara ni mkapa na makongoro unatevemea nini.
 
No one is 100% perfect,the most important thing is to calculate the risk involved.

Pia inasemekana hata Sumaye na Lowasa wamenunua hizo nyumba, na Wao muwa apprehend kama kuuza ni ishu.

Pia Sumaye alitoa ufafanuzi, kuuza nyumba za serikali haukuwa uamuzi binafsi, sumaye na Lowasa walikuwepo kwenye maamuzi ya kuuza nyumba.

Usiwe bias unapojadili mambo

Hakuna anaelalamikia kuhusu uuzwaji wa nyumba, hilo tunajua ni kosa la serikali nzima ya awamu ya kipara na adunje, hoja ni utaratibu wa kuziuza.

1. Aliepewa mamlaka ya kuuza hakuwa waziri wala wizara, ilipewa Tanzania Building Agency maana ndie msimamizi wa ujenzi wa nyumba za serikali, kwa hiyo walipewa kama independent body kusimamia uuzaji wa nyimba. Magufuri akaingilia uuzaji wa nyumba wakati hakua amepewa mamlaka kuuza, yeye akawa ndio anataka nani auziwe na nani asiuziwe, nani auziwe bei gani na nani asiuziwe.

Mfano, nyumba ya bilioni moja yeye akaithaminisha ni milioni 52 na akaamuru apewe hosea wa Takukuru, yeye sio mthaminishaji wa majengo na hakupewa hiyo kazi. Nyumba ya bilioni 1.5 akamuuzia hawala yake milioni 22.

2. Sheria ya uuzaji ilitaka atakaeuziwa kwamnza awe mtumishi wa umma, yaani ana mkataba au barua ya ajira rasmi toka serikalini, pili awe ni senior kama hakimu wa wilaya,sijui nani wale wote mabosi bosi lakini alimuuzia mpenzi wake hakua mtumishi wa umma ukiachia usenior, mdogo wake hakua senior alikua intern tu bado hata hajapata barua ya uthibitisho kazini.

3. Magufuri alimuuzia makamo mwenyekiti wa sasa wa ccm mangula nyumba na baadhi ya wakuu wa wilaya, mangula hakua mtumishi wa umma, alikua katibu wa ccm.

Magufuri hafai kua rais na hawezi kua rais wa taifa lolote lile.
 
sasa kama una ushahidi,unasubiri nini kuupeleka mahakamani badala ya kupoteza muda humu jf?

Mimi sio dola, ni raia tu, naishangaa ccm na serikali yake yenye wajibu wa kuwapeleka waovu mahakamani inawachekea tu. Hovyo tu. Ok lakini pengine naongea na layman asiyejua hata mfumo wa sheria na mahakama unavyofanya kazi.
 
Duh hii habari sijui jaji warioba hajaiona mana ule wimbo wake wa uadilifu naona angeutafutia chorus nyngne
 
Wasema nyumba 8,000 kauza kwa mkono wake mwenyewe
-Apuuza maonyo ya wataalamu
-Mafaili ya Sundi na Musa aliyabeba kwapani


ALIYEKUWA Waziri wa Ujenzi, John Magufuli, katika Serikali ya awamu ya tatu, aliteka madaraka na kuwa mwenyekiti wa zoezi la kuuza nyumba za serikali ambazo hadi sasa, zimeshauzwa 8,288 imefahamika.

Habari zilizopatikana ndani ya wakala wa Majengo ya Serikali (TBA), zimethibitishia Rai wiki hii kwamba Magufuli alihakikisha anashiriki kama Mwenyekiti katika zoezi zima la kuuza nyumba, ambalo kimsingi lilistahili kusimamiwa na Mtendaji Mkuu wa TBA.

Kwa mujibu wa vyanzo kadhaa vya habari ndani ya TBA, Magufuli alifanya kila aina ya ‘fujo’ katika zoezi la kuuza nyumba hizo, wakati mwingine akibatilisha maamuzi yaliyofanywa na Kamati ya TBA ya kuuza nyumba hizo, akiwapangia watu nyumba kwa utashi wake na wakati mwingine akiwakemea wale wote waliomshauri kinyume na matakwa.

Ni chini ya utaratibu huo, habari zinaeleza kwamba Magufuli, aliyabeba yeye mwenyewe mafaili ya ndugu zake; Musa Magufuli ambaye ni mdogo wake, na Sundi Malomo ambaye ni mzazi mwenzake na kuwalazimisha watendaji wa TBA wafuate matakwa yake katika kuwapatia nyumba ndugu zake hao.

Habari hizo zinaeleza kwamba awali Mtendaji Mkuu wa TBA alimshauri Magufuli kwamba suala la mauzo ya nyumba kwa ndugu zake ni kinyume cha utaratibu. Hata hivyo, imeelezwa kwamba Magufuli alilazimisha huku akisema mdogo wake hana tatizo kwa sababu alikuwa tayari mfanyakazi wa Serikali.

Musa aliajiriwa kwa mkataba wa miezi mitatu, baada ya mwezi mmoja akauziwa nyumba na baada ya miezi miwili akaacha kazi.

“Kwa upande wa Sundi, kwanza ilikuwa Sundi auziwe nyumba moja kwa moja. Lakini Magufuli alipoonywa akashtuka na kusema suala hilo aachiwe yeye mwenyewe. Na ndipo akaibuka na jina la Stanley Manongi kwamba ndiye mnunuzi halisi na baba yake Sundi,” vinasema vyanzo hivyo vya habari, vingine ambavyo vilishiriki moja kwa moja katika mchakato wa uuzaji nyumba hizo.

Habari hizo zinaendelea kueleza kwamba baadaye, Sundi alishtuka akitilia shaka uaminifu wa Manongi, kwamba angeweza kumdhulumu nyumba hiyo.

“Ndipo Magufuli aliibuka na mpango wa Sundi kuwa mtoto wa Manongi na mrithi wake na kisha kwa kuhakikisha kwamba hakuna dhuluma yoyote, mtoto wa Sundi naye akarithishwa na kama mrithi wa pili,” chanzo hicho cha habari kinaeleza.

Chini ya sheria ya Executive Agency Act No. 30 ya mwaka 1997, TBA ilipewa madaraka yote ya kuuza nyumba za Serikali, kujenga nyumba mpya, kuzikarabati zilizopo pamoja na kugawa nyumba za madaraja A, B na C kwa wafanyakazi wa Serikali.

Sheria hiyo inaipa mamlaka ya kipekee ya kufanya shughuli zote bila kuingiliwa na chombo chochote.

Chini ya sheria hiyo, Waziri anaruhusiwa kuteua wajumbe wa bodi ya ushauri watakaomshauri Katibu Mkuu wa Wizara juu ya namna nzuri ya TBA kusimamia mamlaka yake.

Hadi Machi mwaka huu, wajumbe hao walikuwa ni J. Kijazi, E. Lipambila, E. Lugwisha, Msangi, E. Mwakalinga, D. Kisasi, P. Ncheye, F. Werema na A. Bukuku.

Hata hivyo, sheria haitoi nafasi yoyote kwa Waziri kusimamia shughuli za uuzwaji au upangaji wa nyumba za serikali.

Mtendaji Mkuu wa TBA Togolayi Makumba Kimweri, alipoulizwa kupitia kwa Katibu Muhtasi wake, alimwambia mwandishi wa Rai aandike maswali kisha asubiri kuruhusiwa kuingia ndani ya ofisi.

Hata hivyo, baada ya kusubiri kwa muda wa saa moja, mwandishi alipokwenda kuuliza akaambiwa kwamba Kimweri tayari alikwishaondoka ofisini kupitia mlango wa nyuma na asingeweza kurudi ofisini.

Lakini baadhi ya wafanyakazi wa TBA wameiambia Rai kwamba kinachoandikwa kwenye magazeti kuhusu ushiriki wa Magufuli kuuza nyumba za Serikali ni kidogo mno kuliko hali halisi.

Kama ilivyokuwa kwa mdogo wake Musa, waziri Magufuli alishinikiza mtoto wa dada yake anayeitwa James Doto Mgosha auziwe nyumba za serikali kwa kumtengenezea ajira ya muda mfupi katika TANROADS.

Tofauti na Musa, Doto ameuziwa nyumba hiyo kwa jina la mtu mwingine lakini anaishi katika nyumba hiyo, namba 64 iliyopo Kinondoni Flats.

Habari kutoka TBA zinaonyesha jina la mtu mwingine (tunalihifadhi) kuwa ndiye aliyeuziwa nyumba hiyo mtu huyo alipata kupitia utaratibu wa Magufuli kupeleka jina lake kwenye wakala wa majengo na kulazimisha apewe nyumba.

Alipoulizwa kwa njia ya simu, Doto alisema suala la ajira na nyumba waulizwe waliomwajiri na kumpa nyumba. Akakata simu.

Mfanyakazi mwingine alieleza Rai kwamba msichana mwingine (jina tunalihifadhi) akiwa na miezi minne tu kazini alipelekwa na Magufuli katika Wakala wa Majengo akilazimisha auziwe nyumba hata kabla ya kuthibitishwa kazini. Nyumba hiyo iko Block A, Ocean Road.

Hata hivyo, habari hizo zinaeleza kwamba msichana huyo ambaye hadi sasa anaishi na wazazi wake, ameipangisha nyumba hiyo kwa mfanyakazi mmoja wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa na analipwa kwa dola za kimarekani.

“Kuuza nyumba za serikali sawa, lakini kweli katika mtindo huu? Sisi tunaoshiriki kuzikagua na kuziratibu tukiomba hatupati, lakini wengine wanaingia serikalini miezi miwili wanapata nyumba. Na wengine hata si wafanyakazi, wanapata, hii si sahihi, alilalamika mfanyakazi mmoja aliyeandikia Rai kwa njia ya barua pepe.

Hadi Machi mwaka huu Wakala wa Majengo wa Serikali (TBA) walishauza nyumba 8,288 ambazo hata hivyo zilitakiwa kuuzwa kwa watumishi wa serikali.

Katika mauzo hayo, Serikali ilitarajia kupata jumla ya shilingi 60,016,556,439.00. Hata hivyo hadi sasa Serikali imepata shilingi 22,684,108,115.08.

Kwa sasa, Serikali imebakiwa na nyumba 1,098 zinazosimamiwa na TBA. Kati ya hizo, nyumba 692 zimetengwa kwa wafanyakazi wa Serikali, nyumba 675 kama tied quarters, nyumba 111 zinatumika kama Rest House za Serikali, wakati nyumba 40 zinatumika kama state lodges. Nyumba 24 zinatumika kama ofisi na nyingine 29 ni kama karakana na bohari.



Chanzo: Rai Nguvu ya Hoja: Toleo Namba 682
🙂🙂
 
Back
Top Bottom