Huyu Magufuli ni mtoto yatima katika familia ya JK. Ni ubishi na kukosa ujasiri kinachomfanya abaki katika serikali ya JK na CCM. Ingekuwa katika nchi zingine kama Kenya, Senegal, Ghana, n.k., huyu mtu angekwisha kujiunga na CHADEMA tangu Julai 2006. Zile makala kwenye gazeti la Rai zilitosha kumuonesha jinsi asivyotakiwa. Katika CCM kuchapa kazi na kusisimamia sheria kama zilivyo ni tatizo. Kwa CCM sheria na taratibu ni kwa walala hoi tu, kitu ambacho Magufuli haelewi. JK alimpa uwaziri kwa sababu za kisiasa, kwani jamii isingemuelewa. Kinachofanyika sasa ni kujaribu kumtoa Magufuli katika nyoa za watanzania ili watakamtema akose wa kumtetea. Na tayari Magufuli polepole ameshaanza kutoka katika nyoa za Watanzania kama tunavyoona humu katika forum. Sasa kwa kukosa ujasiri atasubiri hadi wamtose na aishe kisiasa. Wakimhurumia sana watamuacha hadi kura za maoni za 2010, na hapo inafanyika namna ashindwe. Ndipo atakapoanza kupaparika na kukimbilia katika vyama vya upinzani kama alivyofanya Njelu, but it will be too late, na ataonekana hakubali kushindwa. Katika kundi hili yumo pia Mwandosya. Namhurumia sana Magufuli, maana nathamini utendaji kazi wake.