Kama nilivyokuaidi Mzee Mwanakijiji nimemaliza kusikiliza maoni yako kabla sijasahau napenda kuchukua nafasi hii kuwashauri watu wengine wasikilize pia.
http://mwanakijiji.podOmatic.com/entry/2006-11-12T21_36_01-08_00
Kuhusu magufuli kuandamwa na vyombo vya habari, nadhani ni kweli ni maswala ya kisiasa zaidi nafuatilia litaishia wapi.
Kuna issue ambayo hujaigusia kuna nyumba ambazo zilinunuliwa halafu zikabomolewa ili kujenga nyumba za kisasa wewe unasemaje kuhusu hilo?
Kuna watumishi wa umma walinunua hizo nyumba na baadaye kuwauzia watu wengine na hili tutalitatua vipi?
Na watu wengi walionunua hizi nyumba wame invest (weka hela) kwenye hizo nyumba. Hao watarudishiwa hizo hela au warudishiwe hela walizonunulia?
Mwisho, serikali yetu imeamua kujenga uchumi kwa kutegemea external
investors na hili suala la nyumba ni suala ambalo na wao na wao wanalifuatilia kwani ni wazo toka kwao, je tutawezaji kuwashawishi kuwa tunarudisha nyumba tu hatuwezi kuchukua investments zao mara watakapokuja huku hasa ukizingatia tumeshafanya hivyo mara kadhaa?
Nadhani huu ni wakati muafaka wa kurudisha ile topic yako ya makazi. kama alivyosema mkandara kwenye topic nyingine halmashauri za miji zipewe ruzuku au zimewe ruhusa kukopa kwenye vyombo vya fedha kujenga nyumba za bei rahisi na kuzikodisha na kuweka utaratibu utakaowawezesha watu wasio na makazi kama watumishi wanaoamia miji fulani kupata hizo nyumba kirahisi na hata watu wenye kipato cha chini nadhani hii itakuwa ni muhimu sana katika maendeleo. Halmashauri ya jiji la Dar limeruhusiwa kukopa hela ya jengo la wamachinga 10,000 hivi kila halmashauri inahitaji nyumba 100 nadhani hizo ni nyingi sana. Nadhani serikali irudishe zile nyumba ambazo ni lazima kuwa chini ya serikali kama ile nyumba ya rafiki wako wa Ikulu na hizo nyumba nyingine ziendeshwa na halmashuri za miji. Lazima tukubali makosa yametendeka watu waliohusika kama walivyunja sheria za nchi tunajua kitu cha kuwafanya na kama yalikuwa makosa ya utendaji, hawawezi kazi zao wote waondolewe.