Ndugu sikia hii!
Mazengo secondary iliyopo dodoma kwa sasa chuo kikuu na nyingine nyingi unazozijua ziwe mfano.
Kanisa limeenea karibu sehemu nyingi za nchi hivyo sifikirii kama lipo tayari kuona members wake wanakosa huduma za kijamii kama vile maji,nguo,elimu,chakula nk eti tu kwa sababu ya hofu uliyonayo wewe ya ku monopoly.
Kwa wanaofuatilia historia wanaweza jua kwamba hata mapinduzi ya habari yamechangiwa kwa kiasi kikubwa na kanisa pale radio tumaini ilipokuwa radio ya kwanza binafsi nchini.
Hatutakiwi kuwa na hofu ya maendeleo yanayoletwa na kanisa bali tunatakiwa kuishauri serikali ambayo wewe tena kwa bahati mbaya au nzuri uliipigia kura ijaribu kufanya mambo ambayo yanafanywa na kanisa kwa sasa kama vile kuchimba visima kujenga shule za kutosha na hosptali ili kuondoa mzigo mkubwa kwa kanisa.
Pamoja na yote hayo Kanisa pia linatakiwa kufanya hayo kwa lengo moja la kuisaidia jamii na si vinginevyo na huu ni wakati mzuri kwa kila taasisi kuhakikisha inafanya iwezavyo kusaidia kupunguza matatizo yanayowakabili members wake.
Tukiogopa ya kanisa basi hata JF Monopoly and Expansion INAWEZA IKAWA TISHIO SIKU SI NYINGI TENA HATA KUUNDA SERIKALI YAKE so mimi sioni sababu ya kuwa na hofu katika hili,mfano JF tayari kuna saccos badae kuna jumuiya ya wasio na ajira nimesikia kuna watu wanashamba kubwa tu,vp kama tutamchagua Rais wa JF Tukampta na Prime mister wetu hapo napo hofu yako itapimwa na nini?
Mimi na filiri ni bora ya vyou,hosptali kwani huduma zitolewazo hazibagui dini,jinsia na rangi kuliko kuwa na misikiti ya kina kanali gadafi kila pembe ya nchi tena mbaya zaidi hadi kwenye viwanda na kwenye huduma nyingine za kijamii kama vile petro station mbalimbali(mtoa mada hili ulitakiwa kujengea hofu kabisa kwani halitutendei haki wengine,ama ni kusema hizo sheli na viwanda ni maalumu kwa sisi wenye vikofia vyeupe tuuu??? vipi kama wenzetu wakisusia bidhaa zetu????kama ni hivyo jengeni basi pembeni na makanisa basi tuone hou usawa basi kuliko huu ubaguzi wa wazi huku tukipinga maendeleo thabiti yanayoletwa na kuchangiwa na kanisa tena bila ubaguzi wowote.
Tafakari,jadili na uchangie.