Katika hali isiyo ya kawaida, jeshi la Umoja wa Mataifa nchini Congo, MONUSCO, limekili kuiunga mkono serikali ya DRC katika mapigano yanayoendelea mashariki mwa nchi hiyo.
MONUSCO ilikuwa na kambi ya kijeshi katika mji mdogo wa SAKE, uliopo Km 20 kutoka mji wa GOMA, huku kambi nyingine kubwa na uongozi vikiwa mjini GOMA. Hapo juzi baada ya mapigano makali, ambayo yameuzingira mji huo wa GOMA, MONUSCO ililazimika kuondoa kambi hiyo na kurudi GOMA mjini.
Baada ya siku moja, ndipo jeshi la DRC, washirika wake ambao ni kundi la wakongo lijulikanalo kama Wazalendo, kundi la wanajeshi wa nchi mbali mbali wenye ngozi nyeupe, na MONUSCO, waliamua kurudi kuikomboa SAKE, na ndipo alipouliwa Gen Chirimwami katika maandalizi hayo.
Soma Pia: Mkuu wa mkoa wa Kivu kasikazini auliwa na M23
Siku za nyuma, kulikuwa na malalamiko ya raia wa DRC waliokuwa wakidai uwepo wa MONUSCO hauna msaada na bora waondoke;mara nyingi walikamatwa na madini kutoka huko walikokuwa kakienda kwenye dolia za kijeshi, na kukingiwa kifua na serikali.
Katika mission zote za UN, wanajeshi hawa huwa na jukumu la kulinda amani ya raia waliopo katika maeneo yenye usalama mdogo, na kujihusisha na mapigano, ni pale tu wanapovamiwa,hivyo hawaruhusiwi kuvamia wao. Safari hii, mambo yamekwenda kinyume, wao wamefuata adui wa serikali na kuacha makazi yao.
Hata hivyo, msemaji mkuu wa kundi la M23 kisiasa, bwana Lawrence Kanyuka, ametangaza kwamba vita ni vya wenyewe kwa wenyewe, hivyo kuwaunga mkono, ni wazi wameingia uwanja wa vita hivyo M23 ina haki ya kujihami. Mpaka sasa,katika mapigano kati ya pande hizo mbili, wanajeshi 3 wa MONUSCO wamejeruhiwa.
Mpaka sasa, mji wa Goma umezingilwa na M23, na njia pekee ya kuingia au kutoka, ni njia ya maji au ya anga tu. Na kundi hilo lilisema kwamba ikitokea zikaingia ndege au boat za siraha, zitashughulikiwa.