Okay! Ulichokimaanisha hapa ni poor management, hili si kosa la itikadi bali jamii. Niaminivyo mm, ubinafsi ndo dhambi kuu kuliko zote. Kama Mungu yupo kweli, hii ndo atakayoanza nayo.
Hata Lucifer aliifanya hii. Niaminivyo bnadamu hafungwi kwa sheria bora hata kamba inaweza ikamdhibiti. Ujamaa ulitakiwa uwe imani na dini ya watu... mtu achomwe kwa ndani kwakuwa mbinafsi, asijifikirie yeye bali jamii.
Hili ndo kosa kuu alilolitenda mwl. Nyerere, aliwaamini watu akasahau kuwa ubinafsi wao ndo ubinadamu wao. Akaziachia taasisi zingine kama dini, shule, mila nk zisihuubiri ujamaa.
Mbona makaka wawili wanaweza wakaendesha kampuni vizuri tu. Ubinafsi uloviua viwanda vyetu unang'oleka kiurahisi tu mkuu.
Nia, sababu, zikiwepo uwezo utapatikana tu. Watu walidahi nguo, simu, radio, na dawa za meno,.walipozipata hawakutosheka. Leo ukiwauliza watu, watasema enzi za mwalimu, waliokuwepo huko waliikataa enzi hizo.
Binadamu kwa asili ni mbinafsi, bila yeye kuwa juu kamwe hatoridhika. Cha msingi hapa ni kumuondolea tu hili pepo la ubinafsi... Buddha alishazitoa kanuni zake.