Kuomba Mungu kila MTU anaweza, kusubiri majibu ndo changamoto lakn kumbuka mambo haya hayaachani "kuomba=kusubiri" ukishindwa kusubiri, umeshindwa kuomba na kinyume chake ni sawa, imani inasimamia vyote, kuomba ni imani na kusubiri ni imani pia, kushindwa kuomba au kushindwa kusubiri ni sawasawa na kukosa imani, ndiyo ni kukosa imani kwa yule unaemuomba, kwani yeye husikia kila ombi na hujibu maombi yote, yote kabisa, ndiyo yeye hujibu maombi yote kwa namna yake na wakati wake, hakawii wala hawahi, anajibu, kupokea majibu pia changamoto nyingine, kwani aweza kutoa sawasawa na ombi lako, hapo kuna hatari ya kuota kiburi cha uzima nakujiona wewe mtenda miujiza kwa kuwa kila unachotamka kinatimia, ukatenda dhambi ya "Lucifer" Mkuu wa Giza, lakini pia aweza kukupa zaidi ya ulivyoomba, ukabaki kuabudu vitu badala ya mtoaji, ukavunja amri ya Mungu inayokutaka kumwabudu yeye peke yake, na pia anaweza kukawia au kupunguza katika kile ulichoomba, wewe ukanyong'onyea, ukasononeka, ukakosa imani na kurudi nyuma, ukavunja kabisa nguzo ya uadilifu yaani kukosa Tumaini, ili kuwa tayari kukabili changamoto hizi za sala na makandokando yake, fadhila ya "unyenyekevu" ni ya lazima sana, hii ni fadhila inayomfanya muombaji "kumwachia Mungu awe yote katika yote" Barikiwa.