More than serious nahitaji mume wandugu

Jamani someni tangazo vzr muelewe. Dada wa watu kasema ana miaka 32 na anatafuta mwanaume mwenye umri ulio range 33-34.
 
Umetumia ujana wako weehh afu unarudi huku na masharti lukuki. Wachumba walikuja ata 20s ukawaona maboya sasa zamu yako.
 
Utapata mgane hapa vijana utasubiri mno..!
 
Sijaku-PM maana sina vigezo...bali nakuombea kwa Mwenyezi Mungu akupe mume bora kama kweli unamaanisha kuhitaji na kutulia naye mjenge familia.
 
 
Embu tupe sababu za wewe kuchelewa kuwa na mwenza mpaka sasa? Umekuwa unachagua saana ( so selective ) na sasa imekuwa too late Yale ya ndege mjanja huishia ktk tundu bovu au nini kimekuwa na wewe for all the time kuamini JF utampata MTU ukiona jibu lako liko so private ni PM
 
Je utakuwa tayari baada ya kupima kubeba mimba kabla ya ndoa,maana Siku hizi mimba tabu
 
Kudadeki! Wee ni nouma sana, nimependa majibu yako. Mtu anatafutaje mume wa kukuoa kwa kuchunguza tabia zake kwa kutumia darubini? Na huyo atakae kubali kuoa mtu mwenye 32yrs ni nani wakati Mungu wetu siku hizi inaelekea ni kijana.

Maana kwa uumbaji anaofanya Mungu huyu siku hizi nahisi Dada yetu (32) atasubiri sana na hayo masharti yake
 
Hahahahahhaha.... Nimejikuta nacheeeeka mie!!!
 
daah pipoz wengine bwn ujue ujuaji mwingi mbele giza,hujaelewa nini sasa hapo Mkuu!!? # none sense#
 
Nie
 
Mi nina 30 vip pia nina degree karibu inbox zaid
 
Pia napenda sana wanawake walionizid umri
 
Kuomba Mungu kila MTU anaweza, kusubiri majibu ndo changamoto lakn kumbuka mambo haya hayaachani "kuomba=kusubiri" ukishindwa kusubiri, umeshindwa kuomba na kinyume chake ni sawa, imani inasimamia vyote, kuomba ni imani na kusubiri ni imani pia, kushindwa kuomba au kushindwa kusubiri ni sawasawa na kukosa imani, ndiyo ni kukosa imani kwa yule unaemuomba, kwani yeye husikia kila ombi na hujibu maombi yote, yote kabisa, ndiyo yeye hujibu maombi yote kwa namna yake na wakati wake, hakawii wala hawahi, anajibu, kupokea majibu pia changamoto nyingine, kwani aweza kutoa sawasawa na ombi lako, hapo kuna hatari ya kuota kiburi cha uzima nakujiona wewe mtenda miujiza kwa kuwa kila unachotamka kinatimia, ukatenda dhambi ya "Lucifer" Mkuu wa Giza, lakini pia aweza kukupa zaidi ya ulivyoomba, ukabaki kuabudu vitu badala ya mtoaji, ukavunja amri ya Mungu inayokutaka kumwabudu yeye peke yake, na pia anaweza kukawia au kupunguza katika kile ulichoomba, wewe ukanyong'onyea, ukasononeka, ukakosa imani na kurudi nyuma, ukavunja kabisa nguzo ya uadilifu yaani kukosa Tumaini, ili kuwa tayari kukabili changamoto hizi za sala na makandokando yake, fadhila ya "unyenyekevu" ni ya lazima sana, hii ni fadhila inayomfanya muombaji "kumwachia Mungu awe yote katika yote" Barikiwa.
 
ifike hatua JF tukue kiakili, kimwili na kihekima... nijuavyo mimi humu jf wapo wastaarabu kuliko hata mtaani au barabarani... mtu anapokuja na wazo lake hebu liheshimuni basi na kama kwako limekaa vibaya pita tu... hujalazimishwa kumbuka..!!!
naboreka sana.. ni ujinga na upumbavu tu..!!!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…