Mtego wa Noti
JF-Expert Member
- Nov 27, 2010
- 2,591
- 1,616
Inabidi uelewe kiini hasa cha machafuko Kenya 2007 ilikuwa ni nini? Kiini cha machafuko ni mgogoro wa kikabila kati ya Kalenjin na Kikuyu hasa kuhusu Ardhi. Ni wa muda mrefu. Uchaguzi wa 2007 ilikuwa tu ni kichocheo cha mgogoro huo wa muda mrefu ndio maana maafa mengi yalitokea katika eneo la Eldrot ( kalenjin area) kwa vurugu zilizoandaliwa maksudi. Ni kama kule Rwanda baada ya Ndege ya Habyarimana kutunguliwa na kumuua mauaji ya kimbali yalianza sio kwa sababu ya Habyarimana aliuuwawa bali ni chuki ya muda mrefu kati ya Watusi na Wahutu. Kifo cha Rais Habyarimana ilikuwa ni "trigger point" tu kama Uchaguzi wa 2007 Kenya ulivyokuwa "Trigger point " ya mauhaji kule Kenya.
Ocampo amefanya uchunguzi wake na anasema waliohusika kwa undani kabisa ni hawa sasa kwa watu kusema Kibaki na Raila wako wapi is to miss the point.
Mmmmh, anyway!! your argument may be true!!!!