Morocco kujenga Uwanja mkubwa zaidi duniani kwa ajili ya Kombe la Dunia 2030

Morocco kujenga Uwanja mkubwa zaidi duniani kwa ajili ya Kombe la Dunia 2030

Waufukweni

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2024
Posts
5,383
Reaction score
18,776
Wakati Morocco ikiendelea kuandika historia uwanjani katika Kombe la Dunia la FIFA la 2026, inaendelea na mipango mukubwa ya ujenzi wa uwanja baada ya kuwa mwenyeji wa Fainali ya Kombe la Dunia la FIFA ya mwaka 2030.

1784116558523.png
Uwanja wa Grand Stade Hassan II utajengwa katika eneo la El Mansouria, kilomita 38 kaskazini mwa jiji la Casablanca, ikiwa ni sehemu ya maandalizi ya Morocco kwa ajili ya Kombe la Dunia la FIFA 2030, ambalo litaandaliwa pamoja na Hispania na Ureno. Kampuni za usanifu za Populous na Oualalou + Choi ndizo zimebuni mradi huo, unaotarajiwa kuifanya Grand Stade Hassan II kuwa uwanja mkubwa zaidi wa soka duniani.

1784116656267.png
Mradi huo unahusisha eneo lenye ukubwa wa hekta 100, likijumuisha uwanja wa soka, bustani za kisasa pamoja na miundombinu mingine ya michezo. Muundo wa sasa unajumuisha malango makubwa 32 yenye bustani zilizoinuliwa mita 28 kutoka ardhini, pamoja na viti 12,000 vya wageni maalumu (VIP) na huduma za kifahari vilivyopangwa katika ngazi tano.

Soma: FIFA yafikiria uwezekano wa Kombe la Dunia kushirikisha timu 64 ifikapo 2030

Kampuni ya Populous imesema maandalizi ya awali ya ujenzi yalianza baada ya serikali kuidhinisha ufadhili wa mradi huo mwezi Oktoba 2023.

1784116572305.png
 
Tanzania haiwezi kujenga kiwanja kama hicho kwa hali hii ya sasa ambapo nchi inatawaliwa na wafisadi watupu.

Nashangaa Morocco ambayo ukilinganisha na Tanzania kwa rasilimali na hata vivutio tofauti ni kama usiku na mchana lakini vitu wanavyofanya katika nchi yao Tanzania hawawezi kufanya mpaka mwisho wa dahari.

Viwanja vya Morocco kwenye Afcon iliyopita vilikuwa vyenye viwango sawa na Ulaya au Marekani viwanja ambavyo kamwe Tanzania haiwezi kuwa na ndoto ya kumiliki hata siku moja.
 
Kwamba unalinganisha Morocco na Tanzania vivutio? Hebu kuweni serious aisee,
 
Nasubiri wenye chuki na roho mbaya kwa morocco,

Hongereni sana morocco

Tumewalipia huku, jana tumempiga ufaransa goli 2-0....na leo tumempiga Uingereza goli 2-1

Final Argentina 🇦🇷 na 🇪🇸 Spain
 
Labda hujanielewa, yaani Tanzania pamoja na vivutio kibao lakini kimaendeleo Morocco wanatuzidi mbali sana.
Morocco Wana vivutio zaidi yetu, ni katika Nchi yenye vivutio zaidi Africa, kuna Nchi 3 Africa ambazo zinavutia zaidi watu kutembelea, Egypt then Morocco then South Africa.

Google angalau kidogo kuhusu sekta Yao ya Utalii.

Na pia Utalii sio Tu natural resources, Utalii unatengenezwa, hata huo uwanja kama kweli utakua mkubwa zaidi duniani tegemea kupata visitors wengi kuliko hata Mlima Kilimanjaro. Uwanja wa sasa mkubwa Africa FNB wa hapo South Africa, japo si mkubwa Duniani Ila still unavutia makumi kwa maelfu ya watalii kwa mwaka ukiachilia Wanaoenda kuangalia mpira.
 
Back
Top Bottom